FAINALI
ya Sports Extra Ndondo Cup imemalizika leo Jumamosi Julai 30, 2016 kwa
timu ya Temeke Market kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kauzu FC
mchezo uliopigwa katika dimba la Uwanja wa Bandari (Wembly), Jijini Dar
es salaam.
Mchezo huo umeshuhudia timu ya Temeke Market ikiibuka
mabingwa kwa kuwafunga Kauzu FC ambapo Mabao ya Temeke Market
yalifungwa na Ramadhan Madebe, Shaban Kisiga na Adam Kingwande huku lile
la Kauzu FC likifungwa na Rashid Tumbo.
Kwa kutwaa ubingwa huo Temeke Market wamejitwalia
kombe pamoja na shilingi milioni 10 huku wakitoa mchezaji bora wa
mashindano hayo ambaye Shaban Kisiga aliyejinyakulia kitita cha shilingi
milioni moja, viatu na tuzo.
Kisiga amesema kuwa anafurahi kuona kuwa amekuwa
mchezaji bora kwa mara ya pili mfululizo na ametaka waandaaji wa
mashindano haya waboreshe zaidi ikiwemo kukarabati viwanja
vitajavyotumika.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mgeni Rasmi katika Fainali hiyo, alikuwa ni Waziri
wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye (katikati) alieambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine. Pichani ni Timu iliyoshika nafasi ya pili ikipita kukabidhiwa zawadi yao ikiwa ni mfano wa hundi yenye kiasi cha shilingi milioni tano kutoka kwa Kampuni ya Simu ya Airatel Tanzania, iliyokabidhiwa na Meneja Mawasiliano wake, Jackson Mmbando.
Nyanda
wa Timu ya Kauzu FC akiondoa hatari iliyoelekezwa langoni kwake katika
Mtanange wa Fainali kati ya Timu hiyo na Temeke Market iliyoibuka na
Ubingwa wa Mashindano ya Ndondo Cup 2016.
Chenga ya mwili.
Mchezaji wa Temeke Market akiwania Mpira wa Juu mbele ya Beki wa Kauzu FC.
Mambo yalivyokuwa baada ya kuruka.
mchangani hiyo!
ReplyDelete