Kama
Kristo alivyokufa na kufufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu
atawaleta pamoja naye I The. 4:14
Famila ya Bw. Barnaba Leo Kidulile wa Mbezi beach, Dar
es Salaam tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na
majirani wote kwa maombi pamoja na msaada wenu wa hali na mali mliotoa katika
kufanikisha mazishi ya mama yetu mpendwa Anna Mary Kidulile (pichani) aliyeitwa na Mungu
tarehe 28/02/2016 katika Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa tarehe 02/3/2016
makaburi ya Ununio Tegeta – Dar es salaam.
Tunapenda kutoa shukrani za pekee kwa Familia ya Bw. E.P Mkwawa, Familia ya Bw. S. Ezekiel, Familia
ya Bw. J. Mapunda, Familia ya Bw. B. Kimwaga na Familia ya Bw. F. Kayombo, Wana
Ludewa, Mufindi, Nyanyembe na Malangali. Pia tunapenda kutoa shukrani kwa Ukoo
wa kina Kilatu na
Mlyuka, wafanyakazi wa TANESCO, Dar es Salaam Community BANK PLC, PPRA, TRA,
Shule ya Msingi Kunduchi, waalimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili na majirani
wote wa Kilongawima.
Shukrani za pekee ziwaendeee mapadre wa Kanisa la
Anglikana la Mtakatifu Mikael Kunduchi, wana jumuiya ya Mtakatifu Andrea, madaktari
na wauguzi wa hospitali za Regency na Muhimbili.
Kipekee tunapenda kuwaalika ndugu, jamaa na
marafiki pamoja na waumini wote katika ibada ya shukrani itakayofanyika katika
Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Mikael Kunduchi, Dare es Salaam, siku ya Jumamosi
ya tarehe 27 Agosti 2016 saa 3.00 kamili asubuhi na baadae chakula cha mchana.
Ibada hiyo itatanguliwa na mkesha na maombi yatakayofanyika nyumbani kwa Familia ya Barnaba Leo Kidulile Mbezi beach - Mtaa wa Jangwani siku ya Ijumaa tarehe 26 Agosti kuanzia saa 3.00 usiku. Wote Mnakaribishwa.
Ibada hiyo itatanguliwa na mkesha na maombi yatakayofanyika nyumbani kwa Familia ya Barnaba Leo Kidulile Mbezi beach - Mtaa wa Jangwani siku ya Ijumaa tarehe 26 Agosti kuanzia saa 3.00 usiku. Wote Mnakaribishwa.
Heri wenye moyo safi maana
hao watamuona Mungu – Mt.
5:8
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...