Muigizaji Maarufu wa sanaa ya vichekesho kutoka kundi la Orijino Komedi, Emmanual Mgaya a.k.a Masanja Mkadamizaji akishuhudia sebene babkubwa lililokuwa likiporomoshwa na Mkewe Bi. Monica Masatu alikuwa sambamba na Muigizaji mwenzake katika kundi hilo, Isaya Mwakilasa a.k.a Wakuvwanga, katika hafla ya Ndoa yao iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa Primrose, jijini Dar es salaam.Picha zote na Joseph a.k.a Kasampaidadaily
Masanja Mkadamizaji akizungumza jambo huku Mkewe Monica Masatu akisikiliza.
Moja
ya vitu vilivyowavutia watu wengi walioalikwa kwenye mnuso huo, ilikuwa
ni hii show ya wakali hawa wa kuvunja mbavu ambao ni wafanyakazi wenza
wa bwana harusi kutoka kundi la Orijino Komedi yaani hapo namzungumzia
Joti, Wakuvwanja na Profesa. hawa jamaa waliiteka kabisa sherehe hiyo.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Hiyo mikanda (katika vazi mfano wa Polisi nchini) hivi huwa inafungwa tu almuradi au inakuwa na ufungaji unaozingatia mpangilio wa rangi, yaani rangi ipi iwe kwa juu na ipi iishie chini (Kijani-Bluu/Bluu Kijani) mfano bendera yetu ya Taifa inaanza na Kijani na kuishia na Bluu na sio Bluu kuishia Kijani. Japo ni 'Commedy' lakini alama za Taifa popote zinapoonekana kutumika au kuwepo basi ni lazima zipewe heshima yake au zitumike inavyostahili. Ni maoni yangu kama hilo limefahamika.
ReplyDelete