Na John Stephen, MNH
 HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma bora hasa ya vipimo kwa wagonjwa mbalimbali na kufanikiwa kupima wagonjwa 41,101 katika mwaka 2015/2016 kutoka wagonjwa 32,010 waliopimwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Buberwa Aligaesha imeeleza kwamba mashine zinafanya kazi vizuri na kwamba hakuna mashine mbovu hadi kusababisha wagonjwa kukosa huduma za vipimo.

“Hospitali inahakikisha kila mgonjwa anayehitaji vipimo anapata na kwa gharama nafuu. Kama mashine ilisimama kufanya kazi tangu Januari hadu Juni, 2016 ni kwa muda wa kati ya siku moja hadi mbili kupisha matengenezo kinga,” amesema Bwana Aligaesha katika taarifa yake aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari.
 Mgonjwa akiwa katika mashine ya MRI LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Pembeni ya mgonjwa ni Mtaalamu wa Mionzi, Medard Mallya akimsaidia mgonjwa kukaa vizuri kwenye mashine hiyo.
 Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali Ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Flora Lwakatare akifuatilia mgonjwa anavyochukuliwa vipimo leo mchana katika hospitali hiyo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Dah! Kweli Magufuli Oyeeee!!!

    Sasa shughulika na boda boda rais wetu wawe na njia yao pekee ya kupita huko mabarabarani. Ajali zinazosababishwa na hawa jamaa zimezidi hapa Dar Es Salaam. Kila ukikata kona kuna ajali ya boda boda. Maisha ya watu yanakuwa hatarini sana. Wajengee pembeni huko wasiingiliane na magari. Na foleni pia zitapungua sana.
    Thanks in advance.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...