Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara VPL ilifunguliwa rasmi wikiendi
iliyopita kwa mechi 6 kuchezwa katika viwanja tofauti. Katika mechi ya Simba
dhidi ya Ndanda FC tulishuhudia Simba ikipata ushindi wa magoli 3 – 1 huku
winga mpya wa Simba, Shiza Kichuya akifanikiwa kufunga bao zuri kuhitimisha
karamu ya magoli 3.
Nae kocha mkuu wa klabu ya Azam FC
ambayo mwaka huu imefanikiwa kuchukua Ngao ya Jamii alisema kuwa anahitaji muda zaidi ili kukisuka kikosi chake na
kucheza kupitia mifumo wanayoendelea kuwafundisha wachezaji wa timu hiyo.
“Kwa
sasa tunafanya tathmini ya mchezo uliopita, kutoa makosa na kurekebishana pale
tulipokosea, tukimaliza hapo kwa wiki hii tutaanza kujipanga kwa mchezo ujao
(Majimaji), lakini cha kwanza tunaangalia yali yaliyotokea katika mchezo wa
kwanza, mapungufu yalikuwa wapi na nani anapaswa kufanya nini,” alisema.
Mechi ya Stand United na Mbao FC timu iliyopanda
daraja haikufanikiwa kutoa mshindi na kule Songea timu ya Majimaji ilikubali
kupokea kichapo cha goli 1 – 0 kutoka kwa Tanzania Prisons. Hii leo kutakuwa na
mchezo mmoja utakaochezwa jijini Mwanza ambapo Toto Africans itamenyana na
Mwadui FC. Msimu uliopita mechi mbili za ugenini na nyumbani za timu hizi
ziliisha kwa ushindi wa goli 1 bila huku kila timu ikitamba kwenye uwanja wake.
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita hawakucheza
mechi yao ya ufanguzi ili kupata nafasi ya kujiandaa na mechi ya Shirikisho
dhidi ya TP Mazembe. Yanga itaanza kampeni ya msimu huu hapo Jumamosi kwa
kucheza na African Lyon.
Kwenye picha baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara ya Masoko ya Vodacom Tanzania wakiongozwa na Mkuu wa Idara hiyo Nandi Mwiyombella (katikati) walifika kushuhudia mechi kati ya Simba na Ndanda.
Endele Kufuata kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii ukitumia #VPL2016 uweze kutabiri matokeo ya mechi na kupata taarifa zaidi kuhusu ligi kuu ya Vodacom. Pia kupata live match updates kila wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...