“Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”. Amesema Mh.Masaju.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju alipokuwa akizungumza nao masuala mbalimbali yaliyohusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua masuala mbalimbali kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.PICHA NA MICHUZI JR
Akizungumza
na Waandishi wa habari jijini Dar leo,Masaju amesema kuwa polisi
wamesema kuwa wana hali ya kuzuia mikutano na maandamano iwapo watabaini
kuwa yataibuka mambo yatakayohatarisha amani ya nchi,Masaju amesema
kuwa maandamano hayo yataleta madhara na athari kama maandamano hayo ya
UKUTA-Septemba mosi mwaka huu.
Amesema
kuwa madhara na athari ya maandamano hayo ni kubwa kutokana na siku
hiyo itakuwa mahsusi kwa ajili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ
ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwao,akaonngeza kuwa siku hiyo kutakuwa
na tukio muhimu la kupatwa kwa Jua huko Lujewa mkoani Mbeya ambapo ni
muhimu kwa nchi kupata manufaa kwa Watalii kuja kwa wingi na kuweza
kunufaika Kiuchumi.
Masaju amesema kuwa vyama vya siasa
nchini vinatakiwa kutumia vyema haki zao za msingi zilizoanishwa katika
katiba badala ya kutumia, nguvu, ubabe na kupelekea kutishia hali ya
amani na utulivu iliyopo nchini.
Masaju amesema kuwa kumekuwa na
baadhi ya wanasiasa wanaotoa vitisho vya kuitisha mikutano kinyume na
taratibu za kisheria kwa kisingizio cha haki za kikatiba jambo ambalo
sio kweli.“Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia
kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za
kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni
viashiria vya uvunjifu wa amani”.
Masaju aliwataka Wanasiasa
kuwa wakweli na kuacha kuwapotosha wananchi kuwa wananyimwa haki ya
kufanya mikutano kwani wapo baadhi yao wanaofanya mikutano katika
majimbo yao baada ya Jeshi la Polisi kujidhirisha kwamba kutakuwa na
hali ya amani na utulivu”. Alisema Mhe. Masaju.
Aidha Masaju
alipongeza juhudi zinazofanywa na viongozi mbalimbali wa dini nchini
kwa jitihada wanazofanya za kushauri katika kufika muafaka wa hali ya
kisiasa nchini na kuwashauri kuhubiri amani na utulivu kwa waumini wao.
Akitoa
ufafanuzi wa tamko la baadhi ya vyama vya upinzani kutaka serikali
kuvifuta vyama hivyo Mhe. Masaju alisema kuwa suala hilo ni kinyume na
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu katiba hiyo
inaruhusu mfumo wa vyama vingi.
Amani iliyopo inatosha kwa haki zote kupatikana wala hakuna atakayeivunje hata akiandamana mwaka mzima.
ReplyDeleteMbona mikutano ya siasa imekuwepo tangu 1992 lakini amani haikuvunjika wala watu hawakuacha kazi?
ReplyDeleteInasikitisha kupoteza askari kwa mauwaji.
ReplyDeleteLakini polisi wengi hudhulumu wananchi, hata raisi alitoa hotuba kuwa kuna kesi za kubambikizwa, raia wamechoka, ndo maana jambazi wauwaji waovu wanaonekana kwa wananchi kadhaa kama wanawasadia kisasi. japo nakubali muono huo ni mbaya na mwovu. Lakini polisi wafate ushauri wa raisi.
Rais alizuia mikutano ya kisiasa kwanza kabla ya ukuta na kabla ya zuio la polisi kuzuia ukuta.
ReplyDeleteRais hakuzuia mikutano kwa kukemea ukuta. Ni miongoni mwa mbinu zake za kutekeleza "kauli mbiu" yake ya hapa kazi tu. Ili watu wafanye kazi tu.
Naona Mh mwanasheria umeteleza kidogo hapo uliposema katazo la polisi ni baada ya kupewa habari na polisi kuhusu uvunjifu wa amani. Raia wakiona uongo unafanya waone chadema nafuu. Uko upande wa sheria basi sema kweli, usidhani ukisema ukweli utatumbuliwa. Ukimtetea raisi kwa uongo anaweza kukutumbua yule, hapendi uongo.