Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
MSAJILI
wa vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema
masuala yote ya sintofahamu kwa vyama vya siasa yatatuliwa katika
meza ya majadiliano na si vinginevyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi amesema
kuwa kuna taharuki au hofu ambayo inajengwa kwa wadau wa siasa ambayo
inahitaji kuwepo mazungumzo kutokana na taratibu zinazohusu utawala bora.
Amesema kuwa utawala bora ni kuheshimu miundombinu iliyowekwa kwa kufuata sheria zake na bila kufanya hivyo miundombinu haitakuwa imetendewa haki kwa watu kufanya chochote bila kuangalia misingi iliyowekwa katika miundombinu hiyo.
Amesema kuwa utawala bora ni kuheshimu miundombinu iliyowekwa kwa kufuata sheria zake na bila kufanya hivyo miundombinu haitakuwa imetendewa haki kwa watu kufanya chochote bila kuangalia misingi iliyowekwa katika miundombinu hiyo.
Amesema
kuwa Baraza la vyama vya siasa limeandaa mkutano wa wadau wa vyama vya
siasa pamoja na watu wengine kuweza kuzungumza masuala mbalimbali ambayo
yamejitokeza katika kipindi hiki na kupatiwa ufumbuzi wa
sintofahamu miongoni mwa wadau.
Jaji
Mutungi amesema kuwa baraza la vyama vya siasa linatarajia kukaa
Agosti 29 na 30 kutaka wadau wote waweze kushiriki ili kutafuta suluhu kwa yale ambayo yamejitokeza sambamba na kuyatafutia suluhu
katika kuendelea kulinda amani ya nchi yetu.
Amesema
siku zote watu wanatafuta mwafaka wa jambo lolote katika meza ya
mazungumzo na kupata suluhu katika kulinda amani ya nchi yetu.
Aidha
amesema suala la Chama cha Wananchi (CUF) anaangalia na kuona jinsi
gani anaweza kushauri kutokana na kuwa mlezi wa vyama vyote ambavyo
vimepata usajili katika ofisi yake.
Si kweli kwamba uchaguzi ukiisha marekani eti watu wanaacha mikutano ya siasa. kama hamjui ulizeni watz waishio marekani "tea party" ni nini. Ni republican walizungunguka nchi nzima baada ya obama kushinda. Ili chama kisife wakati wa kusubiri uchaguzi mwengine.
ReplyDeleteKwa tz ambapo vyama vya upinzani bado vichanga lazima paruhusiwe wafanye siasa ili wakuwe na ili ushindani wa kweli uwepo.
mimi nipo marekani ndio lakini marekani siasa zikiish zimeisha wanahamisha mambo yote congress.na kama unasema walizunguka nchi nzima kwa obama basi ilitokea kwa ajiri ni mweusi mbona huko nyuma hawakufanya je umefanya utafiti wa kutoshaÉkinachotokea Tanzania ni chadema wamekuwa very schocked na utendaji wa magufuri walitaka mtu lazy.kumbuka walilelewa vibaya enzi za kikwete.wanatakiwa wabadilishe mind seti huu ni utawala mwingine.mimi nafikiri wangetumia jina jingine kuandamaana hakungekuwa na shida ila neno dikteta kila mtu mwenye akili zake anashangaa hii kweli magufuri ni dikteta.maana ya dikteta wanaijua kweli...mmmh naombea tanzania yetu iwe na amani na wanasiasa wasituletee machafuko.jana umeona ndani ya cuf.sasa je chama na chama lazima mkanganiko uwepo ila meza ya mazungumzo iwepo raisi ni wa watu wote.kwahiyo ni vema kukaa chini na chadema kuongea sio kila mtu mmbabe
ReplyDeleteWe jamaa, data ya kuwa kina Sara Palin na wengine kurunguka nchi nzima wakihubiri Obama awe One term only inatosha kuonyesha kwamba bado mahubiri ya siasa yanaendelea mtaani. Mbona Obama hakuwakataza na kuwaambia kuwa tayari kuna congress na senate acheni siasa? Inaonyesha uhuru wa siasa lazima uheshimiwe. Kama katiba haisemi kusubiri uchaguzi basi siasa saa yeyote ruksa.
ReplyDeleteUnajuwa kusema watu wasifanye siasa wafanye kazi si kosa. Lakini kuna jumamosi na jumapili watu wanaweza fanya siasa na wasiingilie muda wa kazi za serikali. Kama katiba inatoa haki basi haki wapewe ila wabunge wa ccm wapitishe sheria ya kuzuia mikutano basi kila mtu ataitii sheria hiyo.
ReplyDeleteJaji kasema sheria zipo ili zifuatwe. Na wote. Kama kuna sheria inatoa uhuru wa mikutano ya hadhara basi raisi na wenzie watii sheria hiyo. Kama sheria hiyo haipo basi chadema watii amri halali ya raisi.
ReplyDeleteJaji, utawala bora ni serikali kutawala vizuri zaidi kisheria. Suala la watu kutii sheria sio la utawala bora ni la mahakama na polisi kusimamia. mahakama itoe kauli nani ana haki kati ya raisi au chadema. Manake lazima kuna mmoja yuko sahihi na mwengine anakosea hapa. Haiwezekani wote wawe sahihi.
ReplyDelete