Na Bashir Yakub.
Kampuni ya umma ndio huitwa public company kwa kiingereza. Kampuni hii
hutofautishwa na kampuni binafsi (private company). Zote ni kampuni kwa
ajili ya biashara na mara zote hutegemea unahitaji kufanya nini ili ujue ni
kampuni ipi uunde.
1.JE KAMPUNI YA UMMA INAWEZA KUMILIKIWA NA WATU BINAFSI.
Ndio inawezekana. Watu wengi hudhani kwa kuwa jina la kampuni hii ni
UMMA basi hudhani ni kampuni ambazo huundwa na serikali. Neno umma ni
jina na limetokana na namna muundo wa kampuni yenyewe ulivyo ,
yumkini halina uhusiano wowote na kampuni za namna hii kumilikiwa na
serikali.
Hivyo yafaa ifahamike kuwa hata wewe mtu binafsi mjasiriamali wa kawaida
waweza kuunda kampuni ya namna hii pengine kutokana na faida
zinazotokana na kampuni ya aina hii.
2.KWANINI UUNDE KAMPUNI YA UMMA BADALA YA KAMPUNI BINAFSI.
( a ) Uhuru wa wanahisa. Kampuni ya umma imetoa uhuru mkubwa kwa
wanahisa. Wakati kampuni binafsi inaruhusu kuwa na wanahisa mwisho 50
kampuni ya umma haina ukomo wa idadi ya wanahisa.
Hii ina maana waweza kuwa na wanahisa hata milioni na zaidi. Hakuna
ukomo wa kiwango cha mwisho isipokuwa kuna ukomo wa kiwango cha
chini. Kiwango cha chini yalazimu wanahisa kuanzia wawili.
( b ) Uhuru wa kuuza na kununua hisa. Katika kampuni binafsi hakuna uhuru
wa kununua na kuuza hisa. Katika kampuni binafsi yatakiwa kabla hujauza
hisa zako kwa mtu mwingine upate ridhaa ya wanahisa wenzako. Wakikataa
huwezi kuuza.
Lakini pia huwezi kumuuzia hisa mtu ambaye wanahisa wengine
hawampendi. Yule wanayempenda na kumridhia ndiye huyo unayeweza
kumuuzia tu na si vinginevyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...