Marehemu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Egno Kamilius Komba.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini - CGP. John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Sheria na Utawala wa Magereza - CP(Rtd) Egno Kamilius Komba kilichotokea jana Julai 31, 2016 akiwa nyumbani kwake Mvuti, Chanika Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza anatoa pole kwa Watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...