Timu ambazo zitashiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) zitakabidhiwa vifaa mbalimbali kwa ajili ya msimu mpya wa 2016/17 Alhamis ya wiki hii katika hafla fupi itakaofanyika LAPF tower Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akiongea na Mtandao huu, Matina Nkurlu Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu wa ligi, alisema kuwa zoezi la kukabidhi vifaa  vya michezo kwa msimu ujao utakaotimua vumbi mwezi huu tarehe 20 lipo tayari kabisa na litafanyika tarehe 4 siku ya alhamis .

Alivitaja vifaa vitakavyokabidhiwa kuwa ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, mipira,soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika,vyote kwa pamoja kwa mujibu wa mkataba.

“Vifaa vyote kwa ajili ya ligi ya msimu ujao vipo tayari kilichobakia ni kuvikabidhi siku ya alhamis ili timu ziweze kuendelea na maandalizi mengine kabla ya ligi kuanza mwishoni mwa mwezi August”.Alisema Nkurlu.

Alisema hafla hiyo ya kukabidhi vifaa inatajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Chama Cha Soka,Viongozi wa klabu mbalimbali vinavyoshiriki katika ligi,wachezaji kutoka timu mbalimbali bila kusahau wadau wengine wa soka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...