Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umeamua
kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida kwenda bara ambayo itaondoka Dar es Salaam kila Jumapili, safari ya kwanza
itakuwa Jumapili hii ya Septemba 04,
2016 saa 9 alasiri.
Taarifa imeainisha kuwa treni hiyo ya huduma
ya kawaida itakuwa na mabehewa 12
kutokea Dar es
Salaam ikiwa na mabehewa manane ya daraja la 3, mawili daraja la pili
kulala na mawili daraja la kwanza. Katika
stesheni za Morogoro na Dodoma yataongezwa mabehewa mawili mawili ya daraja la 3.
Aidha treni ya Deluxe imebadilishwa siku ya
kuondoka badala ya Jumapili kwa sasa kuanzia Septemba Mosi, 2016 itakuwa inaondoka
siku ya Alhamis saa 2 asubuhi kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam.
Halikadhalika mabadiliko haya pia yataongeza
safari za treni ya kwenda Mpanda kutoka Tabora badala ya 2 za sasa zitakuwa 3
kwa wiki ambazo ni Jumatatu, Jumatano na Jumamosi..
Wakati huohuo Uongozi wa TRL umefanya uamuzi wa kihistoria
wa kupeleka huduma za kuuzwa tiketi za
safari zake mjini Kasulu ambapo kuanzia Septemba
Mosi itafungua kituo cha Reli ambacho kitafanya kazi ya kuto huduma hiyo kwa wasafari wanaotoka Kasulu mjini na maeneo ya
jirani . Kwa uamuzi huo TRL imetoa nafasi za tiketi za behewa moja la daraja la 3. Mpango pia uko mbioni
wa kufungua kituo kama hicho siku zijazo mjini
Kibondo hali itakaporuhusu kulingana na mahitaji halisi ya abiria.
Taarifa imesisitiza kuwataka wasafiri na
wananchi kwa jumla nchini hususan wale
wa Mpanda na Kibondo kutumia fursa ya kuongezewa safari na huduma kuletewa
karibu kwa kufuata sheria , taratibu na
kanuni ili hatua iliyochukuliwa na TRL iwe na tija iliokusudiwa.
Aidha taarifa zaidi zinaarifu kuwa hatimaye TRL
imefanikiwa kuongeza mabehewa mawili zaidi ya treni ya Pugu na kufikia idadi ya
behewa 18 hadi jana Agosti 22, 2016. Ni matarajio ya Uongozi ifikapo Agosti 31,
2016 treni hiyo ya Jiji itakuwa na
mabehewa 20 iloahidi ili kupunguza msongamano unaosababishwa na abiria kuwa
wengi katika safari mbili za awali katika awamu zote 2 ya asubuhi na ya jioni.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Focus Makoye Sahani,
Dar es Salaam,
Agosti 23, 2016.
Licha ya TRL kufungua kituo cha kukata tiketi mjini Kasulu,ni bora shirika likaingia katika teknolojia ya kukata tiketi kwa njia ya mitandao ya kipesa ili kuzima kabisa mianya ya rushwa. Stakabadhi za EFD zitumike kama ticketi.Shirika la reli ni moja ya mashirika lenye harufu ya rushwa hasa upande wa tiketi.
ReplyDelete