Naibu
Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea
na wataalam wa Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu
hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano
Prof. Faustine Kamuzora akiongea na
wataalam wa Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao
uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea
na wanahabari hawapo pichani wakati wa
uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es
Salaam leo. (Picha zote na Benjamin
Sawe).
Na abushehe
Nondo,MAELEZO.
Naibu Waziri wa Ujenzi
,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ameiagiza Tume ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano nchini
kuhakikisha wanatengeneza misingi ya uadilifu wa kitaaluma na misingi hiyo
itumike kuwadhibiti wale ambao wanatumia utaalamu huo kwa nia ovu.
Mhandisi Ngonyani
aliyasema hayo wakati akizindua mkutano
wa kwanza ambao umeandaliwa ma Tume mpya ya Teknolojia Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alisema Mkutano huo una
lengo la kuwakutanisha wataalamu wa TEHAMA kutoka katika sekta za umma na sekta
binafsi ili kuweza kujadiliana ni kwa namna gani taaluma hiyo inavyoweza
kutumika zaidi kwa faida ya ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
“Wapo baadhi ya watu
wanatumia taaluma ya TEHAMA kwa manufaa mbalimbali ya kujenga uchumi na
maendeleo, lakini wapo wachache ambao wanatumia utaalamu wao kwa manufaa binafsi ikiwemo kuwadhalilisha watu wengine
na kuwaibia fedha zao katika mitandao” Alisema Mhandisi Ngonyani.
Alisema Tume hiyo ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
inatakiwa kuja na sheria kali ambazo
zitawabana wale wote ambao wamekua na tabia ya kutumia mitandao katika kufanya
vitendo viovu badala ya kutumia katika kujiletea maendeleo.
Awali akizungumza
katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Prof.
Faustin Kamuzora alisema uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini ni jitihada za makusudi za
serikali katika kukuza Mawasiliano .
Prof,Kamuzora alisema
kuwa tume hiyo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa na hivyo
kuwasihi watendaji hao kuwaelimisha zaidi wananchi kujikita zaidi katika kufuata maadili ya
taaluma hiyo ili kulifikisha Taifa katika mafanikio ya sekta ya mawasiliano.
Alisema Tume ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano itasaidia kukuza uchumi wa Taifa kutokana
na kukua kwa sekta ya TEHAMA na kuchochea uzalishaji ,ukuaji wa sekta zingine
kiuchumi na usambazaji wa huduma za jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...