Watumiaji wa mabasi ya mwendo kasi warahisishiwa jinsi ya kulipia kadi zao za kusafiria,Haya yametokana na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kuingia ubia na kampuni ya Maxcom Africa kwa kuhakikisha kutoa huduma zilizobora kwa watumiaji wote wanaotumia usafiri huo  kwa kuweza kuongeza Salio kwenye kadi zao za kusafiria za DART kwa urahisi zaidi kupitia huduma ya M PESA . Huduma hii imeanza rasmi tarehe 1 Agosti 2016 inayowalenga watumiaji wote wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es salaam.

Akiongelea huduma hii Sitoyo Lopokoiyit, Afisa mtendaji mkuu wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania, alisema ‘M-Pesa imeongeza wigo zaidi na unafuu kwa watumiaji wa mabasi haya mbali na njia nyingine zilizokuwa zikutumika kama Mawakala wa Maxmalipo au kwenye vituo mbalimbali vya mabasi ya Mwendo kasi (DART). Ushirikiano kati ya Vodaco,  Maxcom na DART ni muendelezo wa juhudi za kuhakikisha kwamba huduma ya M-Pesa inaendelea kumrahisishia na kumboreshea  maisha ya kila siku mtanzania’

Naye Mkurugenzi wa Maxcom Africa ,Juma Rajabu alisema ‘Mfumo uliowekwa na Max malipo kwenye usafiri huu wa Mabasi ya mwendo kasi ni Mfumo wa kisasa  na salama zaidi unaotumia Kadi maalumu pamoja na Tiketi zenye QR codes, pia Mfumo huu umeboreshwa zaidi kwa kuunganishwa na Makampuni za mawasiliano kama Vodacom Tanzania ambapo wasafiri bila kupoteza muda wanaweza kuweka Salio katika kadi zao za kusafiria kupitia huduma iliyo bora nay a uhakika ya M PESA. Kwa mara ya kwanza duniani na Africa kwa ujumla,Vodacom Tanzania inaingia kwenye kitabu cha historia kwa kuwa kampuni ya kizalendo iliyoleta mapinduzi katika Sekta ya Usafiri’

David Mgwassa, Mkurungezi mkuu wa UDART alisema Matumizi ya kadi ni muendelezo wa utambuzi wa Tanzania, kwenye kuelekea maisha ya kisasa. ‘Kadi ya DART inamsaidia abiria kuondoa kero ya kutembea na pesa taslimu na kupanga foleni kwani inamuwezesha kulipia nauli kabla ya safari. Uwezo wa kutumia simu yake ya mkononi unaondoa  usumbufu wa kupanga foleni kwenye vituo vya mabasi ya mwendo haraka. Kizuri zaidi ni kwamba kadi hii inaweza kujazwa kiwango chochote cha fedha kisichozidi shilingi 30,000 kwa wakati mmoja na haina muda wa kikomo wa matumizi na fedha inayokuwa ndani ya kadi itaendelea kuwemo kwenye kadi bila kikomo mpaka mhusika atakapoitumia’

Kuongeza salio kwenye kadi yako DART kupitia M-Pesa fuata hatua rahisi zifuatazo;

1.       Piga *150*00# chagua LIPA KWA M-PESA,
2.       Chagua DART,
3.       Weka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba ya kadi yako ya DART
4.       Weka KIASI (Mfano 2000, 5000, 10000 n.k),
5.       Weka PIN yako ya M-Pesa
6.       Bonyeza 1 kukamilisha muamala. Utapokea ujumbe mfupi kuthibitsha muamala wako.

Aidha, katika hatua nyingine, UDART wameshusha bei ya kadi kutoka shilingi 5,000 ya awali mpaka shilingi 2,000 kwa maana ya bei ya kadi shilingi 500 na nauli ya kuanzia shilingi 1,500.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...