Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha sukari cha Kagera, Ashuwin Rana baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa Agosti 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, Seif Ali Seif .
Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa na Mkewe Mary wakisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa wakati alipotembelea kiwanda hicho Agosti 2, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephene Kebwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa wakati alipokitembelea kiwanda hicho Agosti 2, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
KWA PICHA ZAIDI OFYA HAPA.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amevitaka viwanda vya sukari nchini kuongeza mikakati ya uzalishaji zaidi ili mwaka 2020 Tanzania iwe imefikia kiwango cha kuzalisha asilimia 100 ya mahitaji yake.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 02, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Mtibwa kilichoko mkoani Morogoro ambapo amesisitiza viwanda vya ndani vizalishe zaidi ili kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.
Amesema Serikali imejikita katika kuimarisha na kulinda viwanda vya ndani nchini hivyo ni vema viwanda vya sukari vikaweka mikakati ya kuzalisha kwa wingi ili kuondokana na uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje.
“Kiwango cha mahitaji ya sukari nchini ni zaidi ya tani 400,000, nimeiagiza Bodi ya Sukari kukaa na wataalamu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kufanya utafiti ili tujue mahitaji halisi ya sukari,” alisema.
Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka mkakati wa kulinda viwanda vya ndani kwa kuziongezea kodi bidhaa zinazotoka nje ambazo zinazalishwa na viwanda vya ndani ikiwemo sukari hivyo wenye viwanda hawana budi kuzalisha kwa wingi zaidi.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa viwanda vya sukari nchini kutoa motisha kwa wakulima wa nje kwa kununua miwa yao kwa bei nzuri na kuwalipa kwa wakati ili nao wanufaike na uwepo wa viwanda hivyo na kuwa walinzi wa uwekezaji huo.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano Mwandamizi wa kiwanda hicho, Ibrahim Juma amesema kwa sasa kiwanda kinazalisha tani 20,000 kwa mwaka na wanatarajia kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 70,000 ifikapo mwaka 2021.
Juma alisema uzalishaji wa sukari kiwandani hapo ulipungua kutokana na uingizwaji wa sukari kutoka nje hivyo aliipongeza serikali kwa kudhibiti uingizwaji holela wa sukari kutoka nje jambo litakalosaidia ukuzaji wa viwanda vya ndani.
Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa wameanza upanuzi wa mashamba kiwandani hapo ambapo wanatarajia kuongeza hekta 400,000 lengo likiwa ni kutimiza ndoto ya Serikali ya kuifanya Tanzania ijitosheleze katika uzalishaji wa sukari.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 02, 2016.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...