Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
TIMU
ya Yanga inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Mtibwa Sugar Agosti
08 ikiwa ni maandalizi ya kuendelea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Mo
bejaia unaotarajiwa kupigwa Agosti 13 Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na Mtandao huu, Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit amesema kuwa
mechi hiyo itatumika kwa ajili ya kukiangalia kikosi kabla ya kuelekea
mchezo wao wa kimataifa wa kombe la Shirikisho ambapo wana nafasi ndogo
sana ya kufuzu ila bado hawajakata tama kwani kama wakifanikiwa kushinda
michezo ilioyobaki pia inakuwa ni moja ya nafasi nzuri watakayokuwa
nayo katika kundi A.
Deusdedit
amesema kuwa, kwa sasa wachezaji wanaendelea na mazoezi katika viwanja
vya Gymkhana na wachezaji wote wako vizuri isipokuwa Geofrey Mwashiuya
ambaye bado ana P.O.P ila wengine wameanza mazoezi ua pamoja.
Mbali
na hilo pia katika siku hiyo hiyo, Uongozi wa Yanga umetangaza kuitisha
mkutano mkuu wa wanachama watakaojadili masuala ya ndani ya klabu yao
pamoja na maendeleo kwa ujumla kuelekea ligi kuu na nini cha kufanya
ambapo unatarajiwa kuanza majira ya saa 3 asubuhi katika ukumbi wa
Diamond Jubilee na baadae watajumuika pamoja Uwanja wa Taifa kushuhudia
mtanange huo wa kirafiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...