Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei amefanya ziara katika baadhi ya matawi ya Benki hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam kujionea utendaji kazi na kukabiliana na changamoto zilizopo.
Katika ziara hiyo pamoja na kukagua utendaji kazi, Dk. Kimei pia alitumia fursa hiyo kukutana na kuzungumza na wateja.
Dk. Kimei pia alitembelea ATM za Benki hiyo zilipozo maeneo ya Namanga-Msasani, Mikocheni, Tegeta, Mbezi na Millennium Tower na kuahidi kuwa Benki hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa huduma hiyo inaendelea kuboreshwa ili kufikia mahitaji ya wateja. "Hivi sasa tuna zaidi ya ATMs 400 na tunajipanga kufikisha ATM 500 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Pia aliongeza kuwa "Tumeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ATM zetu zinajazwa pesa kwa wakati ili kuondoa usumbufu wowote kwa wateja wetu" alisema Dk. Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza kwa ziara yake katika baadhi ya matawi ili kujionea utendaji kazi pamoaja na kutembelea ATM za benki hiyo.
Dk. Charles Kimei akitoa fedha katika mashine ya ATM ya eneo la Namanga jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara ya kuangalia utendaji kazi wa baadhi ya matawi ya jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, tawi la Tegeta, Richard Mkakala (kushoto), wakati alipofanya ziara kuangalia utendaji kazi katika baadhi ya matawi ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akizungumza na wateja wa benki hiyo katika tawi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...