Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 12 Septemba, 2016
anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo
pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa
Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa
tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.
Rais Magufuli anafanya ziara
hii ya kwanza nchini Zambia akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Kamati hiyo
inajulikana kwa jina la SADC-Troika.
Dkt. Magufuli
alipokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC-Troika kutoka kwa Rais wa nne Jamhuri ya
Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika
katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland tarehe 01 Septemba, 2016.
Katika
Ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi za
Afrika watakaohudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Mashujaa
Jijini Lusaka.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano, IKULU
Lusaka
11
Septemba, 2016
Tangu achaguliwe Raisi wetu Magufuli anatakiwa kutoa kipaumbele kutembelea majirani zetu wa damu Kenya, Uganda ni majirani na tuko katika jumuiya na tuna historia ya ujirani, na hii haiitaji shuruti wala pressure, ni ustaarabu tu na busara ya uongozi.
ReplyDeleteNi swali tu Kenyatta alishawahi kuja Tanzania just to visit? Akaacha kazi zake na kuja kutembelea Jirani yake?
ReplyDelete