Waratibu
wa michuano ya Rock City Marathon, wametangaza gharama na zawadi zitakazotolewa
kwa washindi wa mchezo huo ambazo kilele
chake kinatarajiwa kuwa Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Akizungumzia
zawadi hizo jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa mbio hizo zinazoandaliwa na
kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na mkoa wa Mwanza Bw
Mathew Kasonta alisema washindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na
wanawake watajinyakulia sh. mil 1.5/-
kila mmoja, sh. 900,000/- kwa washindi
wa pili na sh. 700,000/- kwa washindi wa tatu.
Kwa
upande wa mbio za Kilometa tano ambazo zitaongowa na wakuu wa mikoa ya Mwanza
na Simiyu ambazo pia zitahusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali
(Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, Kasonta alisema
washindi watapatiwa zawadi za heshima kwa makampuni huku pesa zilielekwa
washiriki wenye ulemavu wa ngozi.
“Washindi wa mbio za Kilometa tatu ambazo zipo
mahususi kwa ajili ya wazee watapatiwa sh 50,000/- kwa washindi wa kwanza huku
washindi wa pili na watatu pia watapatiwa pesa taslimu,’’ alisema Kasonta huku
akiongeza kuwa kwa washindi wa mbio za kilometa 2 zitakazohusisha watoto wenye
umri kati ya miaka 7 hadi 10 watapatiwa sh 30,000 kila mmoja.
Zaidi
aliongeza kwamba washindi kwanza kwenye mbio fupi za mita 100, 400, 800 na 1500 ambazo ni
mahususi kwa wanafunzi watapatiwa zawadi y ash 50,000/ kila mmoja (wanaume na
wanawake), sh 30,000 kwa washindi wa pili huku washindi watatu wakiambulia
kiasi cha sh 20,000 kwa kila mmoja.
“Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana
wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea kutuunga mkono kwenye maandalizi haya
yaani kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya
NMB, New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma
Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door alitaja.
Alitoa
wito kwa washiriki zaidi kuendelea kujisajili ili kuthibitisha ushiriki wao
kwenye mbio hizo ambazo mbali na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha hapa nchini
pia zinalenga kupambana na ujangili
pamoja na kutangaza utalii katika katika Ziwa ya Ziwa.
“Kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani
wanaweza kujisajili kwa kuchukua fomu katika vituo kadhaa vikiwemo Ofisi za
michezo wilaya zote za mkoa wa Mwanza, Ofisi zote za riadha mikoa ya Geita,
Simiyu na Shinyanga, Uwanja wa Nyamagana, Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustino Mwanza, Kituo cha michezo Malya, Shule ya
Kimataifa ya Isamilo, Mwanza Hotel.
“Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki
pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo
ghorofa ya tatu jengo la ATC, jijini Dar es, Salaam,” alihitimisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...