Hospitali
ya rufaa ya Haydom iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani
Manyara, imepatiwa msaada wa mashuka 100 na benki ya CRDB ambayo
yatatumiwa na wagonjwa wa hospitali hiyo.
Akizungumza
wakati akikabidhi mashuka hayo 100 kwa mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk
Emanuel Nuwass, Meneja wa CRDB Tawi la Babati Ronald Paul alisema
wanatoa msaada huo ili kurudisha hisani kwa jamii.
Paul
alisema wamekabidhi mashuka hayo ili kutoa asante kwa jamii kwenye wiki
ya huduma kwa wateja, kwa kurudisha kwao kile kidogo wanachopata kwa
ajili ya kuboresha mahusiano zaidi baina ya benki hiyo na wateja wake.
“Tutaendelea
kushirikiana na kusaidiana kwenye masuala mbalimbali ya kijamii kwani
tunatambua jitihada na changamoto ya hospitali ya Haydom ambayo inatoa
huduma kwa watu wa Manyara na waliopo mikoa ya jirani,” alisema.
Hata
hivyo, mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk Emanuel Nuwass alisema hii ni
mara ya tatu kwa benki hiyo kutoa msaada kwenye hospitali ya Haydom,
hivyo iendelee kuwa karibu nao kwa ajili ya kupeana ushirikiano wa
kusaidia jamii.
Dk
Nuwass alisema awali benki hiyo ilitoa mchango wa maendeleo wa sh1
milioni kwa ajili ya siku ya Haydom, kisha wakawapa zawadi ya ng’ombe
mmoja mkubwa wa siku ya familia na mashuka 100 yatakayotumiwa na
wagonjwa.
Alisema
hivi karibuni bodi ya hospitali hiyo ilikubaliana na mpango wa malipo
kwa wagonjwa kupitia njia ya kadi ya CRDB na zoezi hilo linatarajia
kuwarahisishia watu wote watakaopata huduma katika eneo hilo la Haydom.
Kwa
upande wake, meneja masoko mwandamizi wa benki hiyo Fredrick Siwale
alisema benki hiyo itandelea kutoa huduma nzuri kwa wateja wao huku
ikiboresha maeneo ambayo huduma haipatikani kwa kuhakikisha wanakuwepo.
“Kupitia
kauli mbiu yetu ya ulipo tupo kama hatupo tutakuja na kama hatujaja
utusubiri, tunalenga kuwahudumia watanzania wote na kupitia hilo ndiyo
sababu tukafika kutoa mashuka haya kwani tunaithamini jamii,” alisema
Siwale.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...