Wataalamu wa Masuala ya Uchumi na Fedha kutoka Tanzania
wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF,
wakifuatilia mazungumzo ya mkutano kati ya Shirika la Fedha Duniani-IMF na
Wizara ya Fedha na Mipango, mkutano uliofanyika katika katika Ofisi za Ubalozi
wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa
na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakiwa katika kikao
cha kazi na uongozi wa juu wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, ambapo masuala
kadhaa yanayohusu hali ya uchumi na maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na
shirika hilo ilijadiliwa, Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa
Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa
kwenye mkutano na Magavana kutoka nchi mbalimbali za kiafrika wanaoshiriki
Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini
Washington DC nchini Marekani, akielezea juu ya ukuaji wa uchumi katika
shughuli za mawasiliano, madini, huduma
ya fedha, bima na huduma za uzalishaji wa viwandani pamoja na changamoto
zilizopo..
Naibu Gavana wa Benki Kuu
Dkt. Natu A. Mwamba akifafanua juu ya changamoto zinazoikumba Tanzania katika
kukuza uchumi hasa katika sekta ya
Elimu, Afya na Miundombinu, akiwa mmoja wa wachokoza mada wengine kutoka nchi
kadhaa za Kiafrika kwenye mkutano uliojadili kuhusu hali ya Afrika, Jijini Washington DC –Marekani.
Baadhi wa wajumbe kutoka
Tanzania waliohudhuria mkutano wa hali ya ukuaji wa uchumi katika Nchi za
Afrika wakati Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania alipokuwa akiwasilisha mada,
Jijini Washington DC-Marekani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha
na Mipango, Bw. Dotto James akiwa na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndullu
wakibadilishana mawazo baada ya kushiriki mikutano ya siku ya Benki ya Dunia na
Shirika la Fedha Duniani-IMF, nje ya ukumbi wa mikutano ya Benki ya Dunia
Jijini Washington DC- Marekani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...