
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikagua uzalishaji katika kiwanda cha Gypsum cha Premalt cha mjini
Dodoma wakati alipokitembelea Oktoba 2, 2016. (Picha na ofisi ya Wairi
Mkuu)
*Aahidi
kufuatilia suala hilo, asema lazima zitozwe kodi kulinda soko la ndani.*Apokea
mchango wa sh. milioni moja kwa ajili ya waliopatwa na maafa Kagera
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atafuatilia ili
ajue chanzo ni kwa nini bidhaa za gypsum zinazoagizwa kutoka nje ya nchi hazitozwi
kodi.
Waziri Mkuu ametoa ahadi hiyo jana jioni (Jumapili, Oktoba 2, 2016)
wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa kiwanda cha Premalt Limited
kinachotengeneza unga wa gypsum
(gypsum powder) aina ya Afri Bond mara baada ya kukagua kiwanda hicho kilichopo
Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu alisema: “Gypsum
inayozalishwa Dodoma ina ubora kama ile inayozalishwa Mchinga, kule Lindi na
hakuna gypsum yenye ubora kama huo
hapa Afrika isipokuwa gypsum ya
Tanzania.”
“Nilikuwa sielewi ni kwa nini gypsum
ya wenzetu ilikuwa inakimbiliwa, lakini sasa nimetambua; ilikuwa na bei nafuu
kwa sababu tumetoa kodi. Sasa hivi, hili jambo nalibeba, naenda
kulishughulikia”.
“Nimeangalia kwenye orodha niliyopewa katika madini yote nimekuta kodi
ya gypsum ni asilimia sifuri. Ni
lazima tuweke kodi ili tutengeneze soko zuri kwa gypsum inayozalishwa hapa nchini. Ni lazima tuweke kodi kwenye
madini yetu mengine kama makaa ya mawe ili tutengeneze soko zuri,” alisema.
Alisema wakazi wa Dodoma wamepata fursa kutokana na uwepo wa kiwanda
kama hicho kwani kiwanda kinahitaji mali ghafi kwa hiyo ni jukumu la wakazi
wake kuchangamkia fursa ya uchimbaji wa madini hayo.
“Natambua kwamba Mkurugenzi wa kampuni hii ataleta mitambo mikubwa zaidi
hivi karibuni. Nendeni benki mkakope ili muweze kununua zana za kuchimbia
madini haya. Yeye ukishafikisha hapa, ananunua ili aanze kusaga na kupata unga
wa gypsum,” alisema.
Alitumia fursa hiyo pia kumpongeza mmiliki wa kampuni ya STJ
Enterprises, Bi. Adella Nungu ambaye ni mmoja wa wajasiriamali wa Kitanzania
wanaotumia gypsum kutoka Dodoma na
kutengeneza mapambo mbalimbali ya kuezekea ndani ya nyumba. Bi. Nungu alikuwepo
kiwandani hapo.
Bi. Nungu alisema anaponunua unga wa gypsum
kutoka Dodoma, kwa wastani anaweza kutengeneza bidhaa za tani 20 hadi 25 kwa
mwezi kutegemea na hali ya soko na oda kutoka kwa wateja wake.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...