Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi
wa Japan nchini, Ian Myles (wapili kulia) wakati Balozi huyo
alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Haji
Janabi, na kulia ni Msaidizi wa Balozi huyo, Pascale Julien. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi
wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kulia) wakati Balozi huyo
alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo
kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania
na Norway. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Balozi wa India
hapa nchini, Sandeep Arya (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea
Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya
kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea zawadi kutoka kwa
Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kulia) mara baada ya Balozi huyo
kumaliza mazungumzo na Waziri ambayo yalifanyika ofisini kwake, jijini
Dar es Salaam leo. Mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kujadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsindikiza Balozi wa
Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao,
yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Lengo
la mazungumzo hayo ni kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya
nchi jirani ya Rwanda na Tanzania. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...