Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeshirikiana na UMOJA
SWITCH ATMS katika kuwawezesha wateja wake wa Airtel Money kufurahia
huduma za kifedha na kutoa pesa kwenye mashine za ATM za UMOJA SWITCH nchi
nzima bila kuwa na kadi ya ATM.
Ushirikiano huu mpya utasaidia kurahisisha huduma za kifedha kwa
watanzania na kuwawezesha kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa
ufanisi zaidi, wateja wa Airtel sasa wanaweza kupata huduma za kifedha wakati
wowote masaa 24 siku 7 za wiki kupitia mashine za UMOJA SWITCH ATMs zilizoendea
nchi nzima
ushirikiano huu pia utasaidia katika kutanua
wigo wa mawakala wa Airtel Money ambapo wateja wa Airtel hawatakuwa na haja ya
kufungua akaunti ya benki wala kuwa na ya kadi ya ATM ili kupata huduma hii,
kwa kupitia mashine za UMOJA SWITCH ATMs mteja ataweza kufanya muamala kutoka
kwenye simu yake ya mkononi na maramoja kutoa pesa zake kwenye mashine ya ATM
kwa gharama nafuu. Kiwango kidogo kitatozwa kama tozo kulingana na kiasi cha
pesa ambacho mteja atatoa.
Meneja Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce akitoa pesa katika mashine za ATM za UMOJA SWITCH mara baada ya kufanya muamala wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Airtel na UMOJA SWITCH utakaowawezesha wateja wa Airtel Money kutoa pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money katika ATMS za Umoja Switch nchi nzima. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa UMOJA SWITCH, Bwana Danford Mbillinyi
Meneja Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa UMOJA SWITCH, Bwana Danford Mbillinyi wakipongezana mara baada ya kuzindua ushirikiano kati ya Airtel na UMOJA SWITCH utakaowawezesha wateja wa Airtel Money kutoa pesa katika kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money katika ATMS za Umoja Switch nchi nzima.
Meneja Kitengo cha Airtel Money, Moses Alphonce akitoa pesa kwenye ATM katika mashine za ATM za UMOJA SWITCH mara baada ya kufanya muamala wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Airtel na UMOJA SWITCH utakaowawezesha wateja wa Airtel Money kutoa pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money katika ATMS za Umoja Switch nchi nzima. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa UMOJA SWITCH, Bwana Danford Mbillinyi. Taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...