Na Anthony John, Globu ya Jamii.
KATIBU Tawala  wa Manispaa ya Ilala Edward Mpogolo amempongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kuwainua wanawake kwa kuwapa nafasi katika nyanja mbali mbali za Uongozi Wa kisiasa na utendaji Wa umma hapa nchini.
Akizungumza katika Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsiakwa mama na watoto Mkoa wa Ilala Mpogolo 
 amesema Rais Magufuli ameweza kuwainua wanawake na kuwa na imani nao hasa katikakazi za kiserikali na kuweza kuwapa uongozi wa juu kwenye sekta tofauti.
 Akielezea ukatili wa kinjisia, Mpogolo amesema kutokana na taarifa zilizofanywa na Shirika la Afya Duniani inaonyesha kuwa Asilimia 15 Hadi 71 waliathirika na ukatili wa kimwili au wa kingono ulifanywa na wanaume au Wenzi wao utafiti ulibaini Pia zaidi ya Asilimia 90 ya waathirika wa ubakaji wanawafahamu wahalifu wao.
Pia aliwataka watoto Wanaoishi katika Wilaya ya Ilala kutokunyamazia vitendo mbali mbali vya ukatili wa kinsia unaofanywa dhidi Yao.
Hata Hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP  Salum Hamdani aliwataka wazazi na watoto kutokunyamazia ukatili wa kijinsia unaofanywa dhidi yao na badala yake kutoa taarifa katika vituo vya Polisi.
Katibu huyo alilishukuru Jeshi la polisi kwa kupitia kamanda wa mkoa wa kipolisi Ilala kwa maandalizi ya kampeni ya siku 16  Ya kupinga ukatili wa kijinsia.

Katibu Tawala wa Ilala  Bw. Edward Mpogolo akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo.

Katibu Tawala wa Ilala  Bw. Edward Mpogolo na Kamanda Hamdani wakienda kukagua shughuli za madawati ya Polisi kuhusu kupinga ukatili wa Jinsia na watoto katika wilaya ya Ilala
Sajenti Doris Gweba wa Dawati la kupambana na ukatili wa kijinsia na watoto Ilala, akitoa maelezo kwa DAS jinsi wanavyofanyakazi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...