Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia), baada ya kuagwa rasmi, katika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimkabidhi zawadi ya shukrani aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia) wakati akiagwa rasmi baada ya kupewa majukumu mengine ya Ukurugenzi Mkuu wa Benki ya AfDB kusini mwa Afrika, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Serikali wakati wa kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero, ambapo alimshukuru kwa jitihada zake katika kusaidia upatokanaji wa mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Barabara, nishati, kilimo na elimu, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero wakifurahia uhusiano mzuri uliopo kati ya Benki ya AfDB na Tanzania ambapo mpaka sasa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo inafikia thamani ya Dola za Marekani Bilioni 2, wakati wa kuagwa kwa Dkt. Kandiero, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...