Na Mdau Kutoka Tanzania-Diaspora,
Hivi karibuni , Mh. Lukuvi alitangaza kiama na wamiliki wa ardhi ambao sio raia. Uamuzi huo wa kufanya hilo zoezi umetutisha sana Diaspora na mtazamo wa Serikali ya 5 kwa Diaspora.
Naelewa sisi Diaspora tuliochukua uraia wa nje tumeukana uraia kisheria. Hilo jambo ni wazi na tunakubali.
But the facts are;
Diaspora tunafikia na kupita Millioni 3 ulimwengu mzima.
Wengi tunahangaika tunasaidia nyumbani, tumetoka familia maskini. Tunasomesha ndugu zetu. Mtu anabeba maboxi masaa 18 kwa siku ili mwisho wa mwezi atume pesa nyumbani kwa ndugu zake.
Wengi tunawekeza Tanzania, cha kwanza ni kununua ardhi, ili tujenge nyumba yakufikia tukirudi. Baadhi yetu tumezika ndugu zetu kwenye hizo ardhi, tumerithi hizo ardhi. Na ndio kitu chetu cha kujivunia.
"Mimi natoka Tanzania na nyumbani nina hii ardhi, na nina mpango wa kuwekeza nifanye maendeleo".
Tunajaribu kuanzisha biashara, na kufanya chochote kuinua familia zetu. Tunahofu kubwa hatuna mtetezi Tanzania, na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Chama ambacho wengi wetu tunakisapoti sana kwa sababu kimejitoa kutufanyia mengi. Na tulikipigania vibaya mno kwenye Uchaguzi 2015 na kubadilisha upepo wa uchaguzi nchini.
Zoezi analofanya Mh. Lukuvi si sawa, ananyanga'nya ardhi za watu ambao wengine wamezika ndugu zao, wamerithi na wamehangakia kuzinunua. Hata kama sisi sio raia kwa kuchukua uraia wa nchi nyingine, mbele ya Mungu zoezi hilo sio la haki.
Napenda kutoa ushauri;
Kwa sasa Mh. Raisi aingilie kati hili zoezi afanye Executive Order;
1.) Kuwasamehe wazaliwa wa Tanzania tu, waliochukua urai mwingine.
2.) Kuwaruhusu kumiliki ardhi ya Tanzania, wazaliwa wa Tanzania tu, waliochukua urai mwingine.
Mpaka hapo sheria mpya itakapotungwa, ili tuweze kuwekeza nyumbani kwa raha na bila shaka.
Tunaipenda sana nchi yetu Tanzania
Na kila pumzi tunayovuta tunajivunia kuwa WaTanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...