Mkurugenzi wa shuke ya sekondari Lord Baden Powell Kanali (kst) Iddy Kipingu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam. Kulia niu Meneja Masoko New Habari Michael Budigile pamoja na mratibu wa mchakato wa uteuzi wa watoto wenye vipaji Michael Mauris.
Na Anthony John,
Globu ya Jamii.
Globu ya Jamii.
IKIWA tunaelekea kwenye uenyeji wa michuano ga soka la vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 mwaka 2019, Kanali Idd kipingu kupitia shule yake ya Lord Barden Powell ameandaa muchuano ga kupata vijana 20 watakaosoma na kucheza mpira katika shule hiyo.
Akizungumza leo hii jijini hapa Dar es salaam wa Mratibu wa mradi huo Michael Maurus, amesema jumla ya vijana 150 wamejitokeza katika mchuano huo na unaotarajiwa kuanza januari1 hadi tareh 3 katika viwanja vya shule hiyo.
"Mbali na maandalizi ya michuano hiyo lakini mradi huo ni mahususi kwa ajili ya kuendeleaza vipaji vya vijana wanaomaliza darasa la saba kujiunga na shule na shule hiyo"amesema.
Kanali mstaafu kipingu amesema kuwa vijana wanaotakiwa katika shule hiyo ni wale wenye umri wa miaka 13 na 14 ambao mpaka michuano hiyo ya vijana ikifika watakuwa wameshakomaa.
" Tunataka vijana wenye vipaji kwani ni jambo la aibu kuona Tanzania tunakuwa wenyeji wa michuano ya vijana, alafu tunashudia kombe likiondoka machoni kwetu, hii sasa basi tunaanza maandalizi mapema" amesema kipingo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...