Jengo la kisasa la Kitegauchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, lililozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Anna Abdallah, ujenzi wa jengo umegharimu sh. Bilioni saba.Mama Anna Abdallah, amesema, jengo hilo limejengwa kwa hali ya juu na limewekwa kila kitu ikiwemo zamani.

"Mpangaji anapotaka kuingia katika nyumba hii, yeye anachopaswa kufanya ni kuja na chakula na nguo tu, halazimiki kuingia na samani yoyote hata TV anaikuta ipo sebuleni", Alisema, Mama Anna. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jengo la kisasa la Kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mama Zakia Megji na Mama Anna Abdallah. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua rasmi jengo hilo. Kushoto kwake ni Mama Anna Abdallah na kulia kwake ni Mama Zakia Meghji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...