WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema amekabidhi pikipiki 200 zenye thamani yash.
milioni 400 kwa vijana 200 wa Jiji la Arusha, ili kuweza kuwakwamua kiuchumi
vijana hao ambao walikuwa
wakiendesha pikipiki za watu ambazo hazina tija.
Pikipiki hizo zimechangwa
na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani Arusha baadaya Mkuu wa Mkoa huo
Bw. Mrisho Gambo kubuni mpango huo ambao umewawezesha
vijana kupata pikipiki bila
riba wala dhamana.
Waziri Mkuu alikabidhi
pikipiki hizo jana jioni (Jumamosi, Desemba 3, 2016) marabaada ya kumaliza
kuhutubia maelfu ya wananchi waliohudhutia katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja cha
Sheikh Amri Abeid.
Baada ya kukabidhi pikipiki
hizo, Waziri Mkuu aliwataka vijana kuhakikisha wanakuwawaaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki ziweze kuwasaidia
kuwainua kipato.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alisema mwananchi yeyote hata kama si mtumishi wa umma anawajibu wa kuiheshimu Serikali na kuitumikia. Hivyo aliwataka vijana hao kuwa waadilifu.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alisema mwananchi yeyote hata kama si mtumishi wa umma anawajibu wa kuiheshimu Serikali na kuitumikia. Hivyo aliwataka vijana hao kuwa waadilifu.
“Serikali ya awamu ya tano
imeanza kazi na moja kati ya majukumu yetu ni kuboresha nidhamu ndani na nje ya
Serikali hivyo ni lazima ipate heshima yake,”
“Tumeamua kuwatumikia. Tumeamua
kuwahudumia watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa na kidini na
Mheshimiwa Rais anataka kuona wananchi wake akifurahia Serikali yao,” alisema.
Kwa upande wake Bw, Gambo alisema
pikipiki hizo zilizokabidhiwa kwa vijana hao zimetolewa sanjari na bima kubwa
(Comprehensive Insurance) kwa vijana 200 ambapo kila Kata ilitoa vijana wanane
Katika hatua nyingine Waziri
Mkuu alisema zaidi ya sh. bilioni 800 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi
mbalimbali ya maendeleo mkoani Arusha. Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani
Arusha kwa ziara ya kikazi alisema kati ya fedha hizo sh. bilioni 476 zitatumika
katika ujenzi wa miradi wa maji ili kumaliza kero hiyo.
“Mkoa wa Arusha unakabiliwa na
changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama, hivyo fedha hizo
zinalenga kumaliza tatizo hilo ambalo limechangiwa na uharibifu wa mazingira,” alisema.
Alisema kiasi kingine cha sh.
bilioni 264 kilitolewa ili kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mkoa huo.
“Umeme Arusha hautakiwi kukatikakatika huu ni mji wa utalii. Tanesco imarisheni
mtandao wa usambazaji,”.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipoingia kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kuhutubia mkutano wa hadhara Jumamosi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua kiwanja chenye mgogoro karibuna na soko la Kilombero Arusha ambacho alitangaza katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuwa serikali imekichukuwa na kuliagiza jiji la Arusha liweke mazingira kuwawezesha wafanyabiashara wadogowadogo kuendesha shughuli zao hapo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kofia gumu Roman Mollel ikiwa ni ishara ya kumkabidhi pikipiki katika tukio la kukabidhi pikipiki 200 kwa vijana wa bodboda wa Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abed jijini Arusha , Desemba 4, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Pikipiki Bw. Dennis Shangari katika tukio la kukabidhi pikipiki 200 kwa vijana wa bodaboda kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...