Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 kuelimisha jamii kuzuia ukatili wa kijinsia. WiLDAF inashirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia (MKUKI), wadau wa maendeleo na mashirika mengine kuadhimisha kampeni hizi kitaifa. 

Yafuatayo ni matukio mbalimbali ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili kama yalivyofanyika sehemu mbalimbali nchini Tanzania chini ya kauli mbiu: Funguka! Pinga ukatili wa kijinsia. Elimu salama kwa wote. 

Maandamano ya amani kupinga ukatili wa kijinsia Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa jiji la Dar es salaam ulianza kwa maandamano ya amani ambapo maelfu walishiriki maandamano hayo kutoka Biafra hadi Millenium towers jijini Dar es salaam. Maandamano hayo yalifanyika tarehe 25 Novemba 2016.
Waziri Ummy Mwalimu mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika tarehe 25 Novemba 2016, jijini Dar es salaam. 

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Ummy alisema serikali ya awamu ya tano imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu salama bila aina yoyote ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu bora bila malipo. "Lengo kuu la elimu bila malipo ni kuhakikisha kuwa watoto wetu hususan wa kike wanapata fursa ya kwenda shule kusoma na kufikia ndoto zao katika maisha." 

Aidha alitoa wito kwa wadau na serikali kwa ujumla kutumia nafasi zao kupinga vitendo vyote vya udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za binadamu vilevile kwa jamii kuwa na malezi bora na kuzingatia maadili kwa watoto na vijana wetu. 

Mama Anne Makinda mgeni rasmi katika kongamano la kitaifa la Haki za Wanawake. Aliyekuwa spika wa Bunge la Tanzania mama Anne Makinda alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kwanza la kitaifa la Haki za wanawake lililofanyika ukumbi wa Millenium Towers jijini Dar es salaam tarehe 28 Novemba 2016. 

Kongamano hilo lililoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la LSF lilikuwa na lengo la kujadili namna mbalimbali za kuwawezesha wanawake kisheria na kiuchumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 

Jamii imeaswa kuhusika kikamilifu katika mapambano ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na salama. Kongamano hilo lilipambwa na kauli mbiu isemayo; Jitambue! Jiamini, Simamia Haki yako. Wageni mbalimbali wanaharakati wa Haki za binadamu walihudhuria kongamano hilo la aina yake wakiwemo Dr. Helen Kijo Bisimba, Mary Rusimbi, Edda Sanga na Dr. Judith Odunga. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...