Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi Kitambulisho cha Taifa cha Wageni, Leonie Schollmeyer (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar leo. Masauni licha ya kupewa elimu kuhusiana na utendaji wa kazi wa ofisi hiyo, pia alizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kwa kuwahudumia wananchi ili kuiletea mamlaka hiyo mafanikio zaidi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akifanya usafi na wanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Masauni alialikwa na Baraza hilo kushiriki kufanya usafi nao na baadaye aliwatembelea wagonjwa wa hospitali hiyo akiwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (hayupo pichani) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas (hayupo pichani).  

 Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) wakimsikiliza Nesi Msaidizi Mkuu wa Wodi ya Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Kichwa katika Hopsitali ya Mnazi Mmoja, Hadia Mmadi, wakati alipokuwa anawafafanulia kuhusu wagonjwa wanavyopasuliwa. Viongozi hao walifanya ziara katika eneo hilo, mara baada ya kufanya usafi mazingira mbalimbali ya hospitalini hapo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto mstari wa mbele), Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar, Hassan Haji Hassan (watatu kulia)  wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya Masauni kumaliza ziara yake ya kikazi kuitembelea Mamlaka hiyo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...