Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kaunda suti) akitoka ndani ya Kituo cha Polisi cha Bububu, Unguja, Zanzibar mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo. Naibu Waziri huyo alitoa agizo kwa Kamishna Hamdan Omar Makame (hayupo pichani) kuwaondoa haraka wamiliki wa miradi mbalimbali iliyopo eneo la Kituo hicho pamoja na katika maeneo mbalimbali ya Jeshi hilo, Zanzibar
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa wa Polisi na Askari wa Usalama Barabarani katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi wa Bomani, Drill Shed, Unguja, Zanzibar. Masauni alilitaka Jeshi hilo, kuwakamata madereva wa magari pamoja na pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani pamoja na kuwachukulia hatua kali.
 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Omar Makame pamoja na Watendaji wengine wa Jeshi hilo, wahakikishe wanawaondoa wamiliki wote wa miradi binafsi katika eneo la Jeshi kwa kuanzia na Kituo cha Polisi Bububu. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo.
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akionyeshwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Bububu, Abdulhalim Ali Haji, mpaka wa Kituo cha Polisi cha Bububu, Unguja, Zanzibar, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo. Masauni alipiga marufuku miradi binafsi iliyozunguka kituo hicho.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...