Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi kabla ya kuzindua Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Chama cha Kuweka na Kukopa (Vicoba-Together) katika sherehe iliyofanyika Skuli ya Chekechea, Miembeni, Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Unguja. Masauni alikichangia chama hicho shilingi milioni tatu.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Redio ya Coconut mjini Unguja, Zanzibar, Ally Dai, jezi kwa ajili ya Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup ambayo yamezinduliwa na kiongozi huyo katika Viwanja vya Matumbaku mjini humo. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiyapokea Maandamano ya timu 38 za Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...