Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewataka vijana nchi kuwa
makini na baadhi ya Mashirika yasiyokuwa ya Serikali ambayo yanajishughulisha
na uhamasishaji wa mapenzi ya jinsia moja (ushoga).
Mhandisi Masauni
alisema, Mashirika hayo hayapaswi kuwepo nchini kwani yanafanya kazi kinyume na
mila na desturi ya nchi yetu na yanapaswa kufutwa haraka iwezekanavyo endapo
yatagundulika.
Akizungumza katika
Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe
Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam,
Mhandisi Masauni aliongeza kuwa, vijana wanapaswa wawe makini katika maisha
yao, kamwe wasikubali kupotoshwa pamoja na kuendeshwa na kundi lolote ambalo
linafanya kazi kinyume na taratibu za nchi.
“Kuna baadhi ya mashirika
ambayo yanajihusisha kwa kutoa elimu na kuhamasisha ndoa za jinsia moja,
mashirika hayo yanafanya kazi kinyume na sheria ya nchi, hivyo tunayachunguza
na tukiyagundua hakuna cha Mswalie Mtume, tutayafuta haraka iwezekanavyo,”
alisema Masauni.
Pia aliwataka
Watanzania kutoa taarifa ya uwepo ya taasisi hizo binafsi zinazofanya shughuli
hizo nchini muda wowote wakizigundua ili zifuatiliwe kwa umakini na hatimaye zifutwe
haraka iwezekanavyo kwa kuwa zinaharibu jina zuri la Tanzania.
Masauni ambaye alikuwa
na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo katika sherehe
hiyo, licha ya kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo kwa kumualika, pia aliwahasa
Waislam nchini wawe na umoja, wapendane na waache kulalamika kwa kuwa
mafundisho ya dini hiyo yanaelekeza mambo mema ambayo kila Muislam anatakiwa
kuyafuata.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa koti)
akiwasili katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika
katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake
Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga
nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Kushoto
ni Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd na Shekhe Mohammed Mussa
(aliyevaa miwani).
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Ziara
ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe
Mahadh Kigamboni, jijini Dar es Salaam
leo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika
ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo
endapo yakigundulika. Kulia kwake ni Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe
Hamid Masoud Jongo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa)
akimsikiliza Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid Masoud Jongo
alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad
Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni, jijini Dar es
Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni, katika hotuba
yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga
nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia aliyekaa) na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Hamid
Masoud Jongo (wapili kulia waliokaa) wakimsikiliza Shekhe wa Wilaya ya
Kigamboni, Abdalla Idd alipokuwa akizungumza na Waislam katika Ziara ya Shekhe Uwesu
bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,
jijini Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo, Mhandisi Masauni,
katika hotuba yake aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo
yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo
yakigundulika.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...