Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ameutaka
uongozi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mkoa wa Morogoro kuhakikisha
wanafanya matengenezo katika barabara zao ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha
mwaka.
Mhandisi Ngonyani ameyasema hayo mara baada ya kukagua barabara ya Ifakara,
Taweta hadi Madeke (KM 225) ambapo amesema barabara ya Ifakara –Kihansi (KM
130) imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea ili kipindi cha
miaka mitano iweze kujengwa kwa lami.
“Katika miaka hii mitano tutahakikisha maandalizi ya awali ya kuwezesha barbara hii
kujengwa kwa kiwango cha cha lami yanakamilika na hivyo kutuwezesha kutenga fedha
kwa ajili ya kuanza ujenzi rasmi”. amesema Mhandisi Ngonyani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Kushoto), akifafanua jambo kwa Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga (Wa tatu kulia), wakati alipokagua barabara ya Ifakara, Taweta hadi Madeke (KM 225) Mkoani Morogoro.
Amesema kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu kwa wakazi wa Ifakara na Kilombero
kwa kuunganisha na Mkoa wa Njombe na hivyo kukamilika kwake zitafungua fursa za
kiuchumi na kibiashara kwa wananchi hao.
Mhandisi Ngonyani amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kutekeleza
ahadi zote zilizotolewa kwa wananchi kwa kuunganisha mikoa mbalimbali kwa ujenzi
wa barabara bora kwa viwango vya lami ili kurahisisha usafiri na kuongeza kasi ya
maendeleo kwa wananchi.
“Serikali ya awamu ya tano ipo madarakani kwa ajili ya wananchi bila kujali itikadi
zao,tumewahaidi kuwaletea maendeleo hivyo tutajenga barabara zote tulizozihaidi kwa
wakati ili wananchi waendelee kunufaika na matunda ya serikali yao”.amesisitiza
Mhandisi Ngonyani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (aliyenyoosha kidole), akizungumza na wananchi wa Mlimba wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro wakati alipokagua barabara ya Ifakara, Taweta hadi Madeke (KM 225).
Ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara yake itaboresha huduma za mawasiliano
katika shemu mbalimbali za nchi ili kuwawezesha wananchi kuwasiliana wakati wowote
ili kukuza mahusiano yao kiuchumi, kibiashara na hivyo kukuza pato lao na la taifa.
“Tumeuomba uongozi wa kila wilaya utuletee maeneo ambayo huduma za mawasiliano
hazijafika au zinasumbua ili sisi tuweze kuzishghulikia na kuzipatia huduma bora za
mawasiliano”. Amesistiza Mhandisi Ngonyani.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga ameishukuru Serikali kwa
uamuzi wa kuiweka barabara hiyo katika mpango wa kuijenga kwa kiwango cha lami
kwa kuwa itafungua fursa mbalimbali kwa wananchi ambo wataweza kusafirisha mazo
yao kwenda katika masokoni kwa urahisi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano yupo Mkoani Morogoro katika ziara
ya kukagua Miundombinu ya barabara, Madaraja na Reli.
Wanakijiji wa kata ya Msagati wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro wakicheza
ngoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani
baada ya kuhakikishiwa barabara ya Ifakara –Kihansi (KM 130) itajengwa kwa kiwango
cha lami.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa tatu
kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mbunge wa Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga (Wa
pili kushoto) kabla ya mkutano na wanakijiji wa Msagati Mkoani Morogoro.
Wanakijiji wa kata ya Msagati wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro wakimsikiliza
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (hayupo
pichani) wakati wa mkutano na wanakijiji hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...