Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi , Marceline Ndimbwa amelazimika kufanyia kazi nje ya ofsi kutokana kukumbwa na majukumu ya kusimamia ujenzi wa madarasa ili kuenenda na kasi ya Rais John Pombe Magufuli aliyemuagiza kumaliza ujenzi huo ndani ya mwezi huu.

Katika hali isiyo ya kawaida Mkurugenzi huyo ambaye ameonekana katika eneo la ujenzi akiendelea na kazi zingine za kiofsi huku akiwa na lundo la mafaili ambayo alikuwa akiyasaini hili kuweza kuruhusu shughuli zingine za kiofisi zikiendelea.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo alipo ulizwa juu ya swala hilo amesema kuwa jambo ni la kawaida katika mazingira ya kazi,kwani jambo moja haliwezi kukwamisha shughuli nyingine zisiendelee wakati wananchi wana mahitaji ya haraka.

Amesema kuwa Rais alimuagiza kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika kwa wakati hivyo yeye kama mteule anahakikisha kuwa anatekeleza agizo hilo kwa wakati hili watu wa Malinyi waweze kunufaika na ahadi za Rais Magufuli.

Amemaliza kwa kutoa wito kwa wakazi wa malinyi kuwa na imani na serikali yao ambayo kipaumbele chake ni kutumikia wanyonge kwa kurekebishe miundombinu ya elimu kwa kipindi kifupi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...