Nteghenjwa Hosseah – Arumeru


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe . Mrisho Mashaka Gambo amemaliza mgogoro wa muda mrefu uliodumu zaidi ya miaka mitatu kati ya Bodi ya Maji ya Makilenga na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga, Kata ya Leburuki Wilayani Arumeru. 

Utatuzi wa mgogoro huo ulifikiwa kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Nkoasenga baada ya Mhe. Gambo kuwashirkisha wananchi wa aneo hilo katika kutatua changamoto hii iliyoathiri wananchi zaidi ya hamsini elfu wa kijiji hiki pamoja na vijiji vingine ishirini na sita vinavyotegemea mradi huo.

Wananchi hawa waliofungiwa maji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa baada ya kufanya uharibifu wa miundombinu ya Maji pamoja na kuweka kinyesi kwenye mabomba walionyesha kuchoshwa na adha hiyo ya kufuata maji umbali mrefu na kwa gharama kubwa zaidi ilihali maji yanapatikana katika Kijiji chao na walionyesha hali ya kutaka muafaka wa jambo hili ili kuendelea kupata huduma ya maji kama ilivyokuwa hapo awali.

Akiongea katika Mkutano huo baada ya mazungumzo na viongozi wa Kijiji pamoja wananchi Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo alisema katika kutoa huduma ya Maji Vijijini tunaongozwa na Sera ya Maji ya mwaka 2002 inayotaka kuchangia hudma za maji na sio kununu Maji hivyo kila kaya inawajibu wa kuchangia kiasi kidogo cha Fedha ili kuwezesha huduma hii iendelee kutolewa siku zote.

“Tunafahamu kwamba maji haya yanaanzia kwenye Kijiji hiki na wakazi wa Nkoasenga ndio walinzi wakuu wa mradi huu na wanastahili kupewa upendeleo wapekee katika kutumia maji haya ili wendelee kutunza mradi huu wa Maji, ni wazi kuwa vijiji vya ukanda wa chini haviwezi kupata Maji endapo tu wana Nkoasenga wataharibu mradi huu wa maji mtiririko”, Alisema Mhe. Gambo.

Aliongeza kuwa umuhimu huu wa nyie kuwa Kijiji mama cha mradi huu hauwapi Kinga ya kutokuchangia gharama za maji, hivyo nataka mniambia mnaweza kuchangia kiasi gani kadiri ya uwezo wenu na baada ya makubalino haya mtalipia gharama za maji kwa mwezi na sio kwa mwaka tena kama mlivyokuwa mnafanya hapo awali”.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (aliyesimama mbele) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadhara
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga wakifurahia makubaliano yaliyofikiwa katika ya Serikali na kijiji hicho ya kulipa Tsh 1500 kwa huduma ya maji mwezi mzima kwa wanaotumia mabomba ya Kijiji .
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makilenga waliohudhuiria kwenye Mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alaxander Mnyeti akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkoasenga kwenye Mkutano wa hadara.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...