Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mwanamuziki mahiri wa muziki wa 'Singeli' na Mchiriku hapa nchini  atambulikae kwa jina la kisanii Msaga Sumu amesema kuwa ameachia singo yake mpya iitwyao Tatizo Nyota, kama zawadi na salamu za kufunga na kufungua mwaka kwa mashabiki wake.

Msaga Sumu amesema hayo katika mahojiano maalumu na mwandishi wa Globu ya jamii kuhusu ni kitu gani ameandaa kwa ajili ya zawadi ya mwaka mpya kwa mashabiki wake.

“sina kitu cha kuwapa zaidi ya hii singo yangu niliyoiachia hivi karibuni ,wimbo huo ambao niumerkodi katika mahadhi ya mchiriku unaojulikana kwa jina la 'Tatizo Nyota', hivyo kila mmoja akae mkao wa kula ili asikilize na kuupa sapoti katika vituo mbalimbali vya radio hapa nchini, ambapo inapigwa pia wanaweza kuipakua nyimbo hiyo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo nimeiweka”amesema Msaga Sumu.

Msaga Sumu amesema kuwa anawashukuru sana mashabiki wake kwa walivyoweza kumpokea katika mwaka huu wa 2016 na kumfanya aonekane kuwa ni moja ya wasanii bora wa muziki wa singeli hapa nchini kwa kupata shoo nyingi na nyimbo zake kufanya vyema katika vituo mbalimbali vya radio.

Aidha hakusita kuwashukuru marafiki zake madereva bodaboda ambao wamekuwa watu wa kwanza kufikisha muziki wa singeli katika masikio ya wananchi kwa kutumia vyombo vyao ambavyo vimefungwa radio zinazo cheza muziki huo muda wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...