Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema
itaendelea kuwaunga mkono watu wenye viwanda ili nchi iweze kufikia malengo ya
uchumi 2020.
Hayo ameyasema
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charle’s Mwijage wakati wa
ufunguzi wa maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mwijage
amesema kuwa watanzania umefika wakati wa kujenga viwanda kuanzia viwanda
vidogo hadi vikubwa kutokana na serikali kuweka mazingira bora katika sekta ya
viwanda.
Waziri Mwijage
amesema kuwa viwanda vidogo sio vya kubeza hata kidogo kwani nchi
mbalimbali duniani zilianza na viwanda vidogo na vikawa vinachangia sehemu
kubwa ya pato la mataifa yao.
Amesema
serikali itavilinda viwanda vilivyopo na vinavyojengwa kutokana na viwanda
hivyo vinaajiri watanzania pamoja na pato la taifa kukua kwa viwanda hivyo, na
ametaka maonesho hayo yalete mafanikio kwa maonesho yajayo.
Mhe. Mwijage
amesema watu walionyesha nia kujenga viwanda ni wengi hivyo matarajio ya nchi
ya viwanda yakawa yameafikiwa na serikali ya awamu ya tano kwa vitendo
Maonesho ya Viwanda vya Tanzania yameandaliwa na
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia taasisi yake ya mamlaka ya
maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kujumuisha viwanda vidogo,
vya kati na vikubwa kushiriki maonesho hayo kwa kwanza ya aina yake kuanzia
tarehe 7 hadi 11 Desemba, 2016 katika viwanja vya (SabaSaba) Mwalimu J.K
Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es salaam. Takriban viwanda 400 vinashikiri na
kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bw. Edwin Rutageruka
yatafanyika kila mwaka wakati kama huu ili kuunga mkono na kusisimua azma ya
Serikali ya awamu ya Tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ili kuongeza kasi ya maendeleo.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charle’s Mwijage akizungumza
katika ufunguzi wa maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya
sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka akizungumza juu maonesho
ya viwanda leo katika viwanja vya Saba Saba barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya hadhira wakimskiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.
Charle’s Mwijage wakati akifungua maonesho hayo katika viwanja vya sabasaba
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charle’s
Mwijage akiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade Bw. Edwin
Rutageruka kutembelea mabanda. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...