Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Paul 'Ben Pol'akizungumza Mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jana usiku akitokea nchini Ujerumani.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ben Paul 'Ben Pol' amefurahishwa na mafanikio aliyoyapata katika onesho lake alilolifanya katika mji wa   Offenbach nchini Ujerumani, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili akitokea nchini Ujerumani, Ben Pol amesema amepata mafanikio makubwa sana katika onesho lake la nchini humo, kwa kupata mashabiki wengi ambao hakuwatarajia.

Ben Pol amesema mafanikio hayo anaweza kusema ni makubwa hasa kwa kufanya onesho la moja kwa moja katika nchini iliyopo nje ya bara la Afrika na kupata mafanikio ya aina hiyo. "Katika maisha yangu ya muziki ni kitu kikubwa ambacho nimeona hata wadau wangu wa muziki niwapte ujumbe kuwa nimefanikiwa na onesho langu hilo na Ujerumani na limenifanya nione kuna mwanga mkubwa kimuziki".

Aidha Poul amesema  hiyo inatokana na kufanya onesho  akiwa msanii pekee yake kwa kutumia vyombo (live band) na haikuwa na waafrika  na wajerumani  walionesha kukubali zaidi hit single yake ya ‘Moyo Mashine’. 

Ameweka wazi na kusema kuwa katika onesho hilo  ilihudhuriwa na watu wanaofikia 10,000 na imeacha historia katika maisha, huku kukiwa na watanzania watatu pekee, yeye mwenyewe, Emmanuel Austin na mjomba wa Emanuel Austin.

Msanii huyo amesema katika maisha yake ya muziki onesho hilo ni la tatu kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki, ikiwa ni pamoja na onesho la Fiesta lililofanyika Dodoma kwa Wabunge wengi kupata jukwanii na onesho lingine lilikuwa usiku wa Mwafrika ambalo nalo lilikuwa na watu wengi.
"Narufahia maisha yangu ya muziki kila siku mashabiki wanakubai nanichofanya na nyimbo zangu zinapendwa kuchezwa kila kona, lakini kubwa kwangu kwenu kila mwanamuziki afurahie kazi yake haswa anapoenda sehemu kukubalika na wenyeji na sio waafrika wenzake ambao uwa wachache ni changamoto ambayo kila mmoja anatakiwa apambane nayo"amesema Ben Pol.

Msanii huyoa anatamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo, Sofia, Moyo Mashine, Nakuchana, Unanichora’ na hivi karibuni ameshirikishwa kwenye wimbo wa msanii Darasa ambao umeshika nafasi kubwa ya kupigwa katika vitu mbalimbali vya radio na televisheni unaitwa Muziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...