Mkuu wa chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST)  Profesa Mark Mwandosya, sambamba na uongozi wa chuo hicho na wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wamezungumzia haja mama ya  kuboresha huduma zitolewazo na  chuo hicho hasa kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wa jinsi zote kwani idadi kubwa ya wanafunzi wa chuo hicho wengi ni jinsia ya kiume.

Profesa mwandosya amesema wakati akihutubia katika Lecture yake ya kwanza chuoni hapo kuwa idadi kubwa ya  watu wanayakimbia masomo ya sayansi na teknolojia kwa dhana ya kuhisi masomo hayo ni magumu haswa kwa jinsia ya kike.
"Masomo yasayansi na teknolojia yanamjenga mtu kiakili na kifikra pia kukupa uwezo mwanafunzi kujiajili pia kuwaajili watu.
"Masomo ya sayansi na teknolojia sio magumu kama ambavyo wengi wanadhani...Uwezo wa kuwapata wanasayansi wazuri wenye kuweza kuwakilisha vizuri ndani na nje ya Tanzania tunao na wakati ni sasa kuwahimiza watoto wetu kuwaandaa vizuri kujifunza sayansi na teknolojia", amesema Profesa Mwandosya.
Mkuu wa chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST)  Profesa Mark Mwandosya akihutubia wanafunzi wa chuo hicho pamoja na wadau mbalimbali kutoka ndani  na nje ya mkoa wa mbeya. 

Profesa Mwandosya akihutubia hadhara katika hutuba aliyokuwa akiitoa kwa wanafunzi na wadau mbalimbali walio hudhuria chuoni hapo katika ukumbi wa Nyerere chuo cha Sayansi na Teknolojia  cha Mbeya (MUST) jijini Mbeya.
Makamu mkuu wa chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Profesa Joseph Msambichaka akizungumza na wadau pamoja na wanafunzi wa chuo hicho.
Baadhi ya wadau na wanafunzi wa MUST wakimsiliza  profesa Mark Mwandosya. PICHA ZOTE NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...