Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea na kumpa pole Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kufuatia
kifo cha Dada yake aitwaye Efrazia Pengo aliyefariki dunia jana tarehe 22
Desemba, 2016 katika Kijiji cha Mwazye, Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa akiwa
na umri wa miaka 79. Mhe. Rais Magufuli
na Mhe. Mama Janeth Magufuli wamemtembelea Kardinali Pengo katika makazi yake
yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakilakiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es
Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, 2016.
Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, 2016.
Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea katika makazi yake yaliyopo Kurasini Jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, 2016. Picha na IKULU





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...