Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI kwa kupitia Waziri wa Nishati na Madini, Mh Sospeter Muhongo, imesema itaendelea kufanya kazi kwa bidii ya kusambaza umeme ili kufikia malengo ya Duniaya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 Watanzania wote waweze kupata nishati hiyo muhimu.Waziri Muhongo aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Alisema usambazaji wa umeme umefanyika kwa kiasi kikubwa lakini bado wanaendelea na miradi ikiwa na lengo la kuwapatia wananchi nishati kwa uhakika kutokana na vyanzo vya nishati vilivyopo hapa nchini.
Profesa Muhongo amesema mradi wa usambazaji wa umeme vijijini umerahisisha upatikanaji wa maendeleo ya haraka kwa Watanzania wengi, hususan wale wanaoishi maeneo ya vijijini ambayo serikali imeendelea kuweka mkazo wa kufikisha huduma hiyo.
Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, alisema kukosekana kwa nishati ya umeme wa uhakika duniani kwa nchi masikini kunawafanya wananchi wakose huduma muhimu kama vile elimu afya pamoja na kufifisha maendeleo ya ukuaji wa sekta binafsi,
Aidha Rodriguez alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kuwezesha nchi zinazoendela ikiwemo Afrika kuwezesha kifedha katika upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuweza kufikia lengo la Dunia 2030.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...