Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),George Simbachawene ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinatunga sheria ndogo ndogo kwa ajili ya uhifadhi vyanzo vya maji, barabara za mamlaka hizo na njia mbaya za kilimo zinazo athiri mazingira.

 Simbachawene ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kibakwe aliyasema hayo  alipotembelea baadhi ya maeneo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa wilayani Mpwapwa ambapo alitembelea kata ya Massa na Ruhundwa katika vijiji vya Mkoleko, Makose, Chogola, Winza, Njia Panda na Ikuyu na alijionea hali halisi ya maendeleo ya wananchi katika vijiji hivyo.

Aidha alibaini kuwapo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na njia mbaya za kilimo katika kijiji cha Mkoleko na kumtaka Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Jabir Shekimweri na timu ya wataalam wa wilaya kuchukua hatua za makusudi kunusuru hali ya mmomonyoko wa udongo unayotishia kutoweka kabisa kwa  kijiji hicho. 

“kamati ya huduma za Jamii ifanye kazi yake, mweke kontua na kuacha kulima na kukata miti katika kingo za makorongo ili kulinda mazingira” alisisitiza Simbachawene. Amewaasa wananchi kutumia fursa za ujio wa makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa kulima mazao ya chakula na biashara kwani miundo mbinu ya lami kutoka Mbande kuja Kongwa, Mpwapwa, Gulwe hadi Kibakwe ujenzi wake unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/2018.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B.Simbachawene (MB) akifafanua juu ya kuanzisha ujenzi wa mradi wa maji ya uhakika wa kisima ambacho mkondo wake umepita chini sana, lakini pia alitoa agizo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutunga sheria ndogo ndogo za matumizi bora ya ardhi na kutojenga au kulima karibu na barabara zinazopita katika maeneo yao.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B.Simbachawene (MB) akikagua maendeleo ya Mradi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Winza (Makao makuu ya kata ya Massa) ambapo asilimia kubwa ya mradi huo ipo katika hatua za mwisho, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mpwapwa Bw. Donald Ng’wenzi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George B.Simbachawene (MB) ambaye pia Mbunge wa Kibakwe akikagua maendeleo ya Mradi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Winza, mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema mwakani.
 Mojawapo ya barabara inasimamiwa na Halmashauri ya wilaya ikiwa imetengenezwa vizuri na kuwezesha uchukuzi wa mazao, bidhaa na watu kuwa rahisi na kuchochea kasi ya maendeleo ya wananchi. Barabara hiyo inaungansha Kata za Massa, Ruhundwa, Rudi na Kibakwe na ipo wilayani Mpwapwa, pia ipo katika Mpango wa pili wa Taifa 2018/2019 kujengwa kwa kiwango cha lami. Awamu ya kwanza ni kutoka Mbande kuja Kongwa, Mpwapwa, Gulwe hadi Kibakwe unaotarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2017/2018
  Sehemu ya ardhi katika kijiji cha Mkoleko, kata ya Massa iliyopo wilayani Mpwapwa ikiwa imeharibiwa vibaya kutokana na njia mbaya za kilimo, eneo lipo katika muinuko na limezungukwa na makorongo yanayopitisha maji kipindi cha masika hali inayosababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na rasilimali misitu na mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...