Na Humphrey Shao,
Globu ya Jamii Morogoro
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa licha ya nchi yetu kuwa na ardhi kubwa na yenye rutuba ya kutosha na hali ya hewa nzuri amesema serikali bado inachangamoto ya uwepo ya ardhi kidogo iliyopimwa na kupatiwa hati hali inayosababisha migogoro.
Amesema hayo kwa waandishi wa habari leo mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuhusu jukumu la vyombo vya habari katika kutoa elimu juu ya sheria ,kanuni na taratibu katika utawala wa ardhi ili kusaidia kutatua migogoro ya ardhi.
“Bado kuna changamoto kadhaa zinazotukabili changamoto hizo ni pamoja na kiasi kidogo kilichopimwa na kupatiwa hati hivyo kuleta migogoro inayohusu umiliki halali wa ardhi baina ya watumiaji mbalimbali wa ardhi” amesema Waziri Lukuvi.
Amesema uelewa duni wamatumizi bora ya ardhi kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na ongezeko kubwa la ardhi kwa ajili ya kuendeleza makazi mijini pamoja na uvamizi wa ardhi katika maeneo yaliyohifadhiwa.
Amesema serikali ya Tanzania inakusudia kutumia fursa ya ukuaji wa uchumi kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka kama ilivyoonekana katika miaka iliyopita katika kuhakikisha maendeleo yanakuwa endelevu na yenye usawa na fursa kwa wananchi wote.
Ameweka wazi kuwa miongoni mwa jitihada zinazoendelea katika kurasimisha sekta ya ardhi na kutekeleza program ya kuwezesha umilikishaji wa ardhi kwa majaribio ya miaka mitatu ambayo inalenga kuleta hati miliki katika wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi katika mkoa wa Morogoro.
Amesema pia program hii itawezesha kufanya mapitio na maboresho ya masula ya kisera, kisheria na kitasisi hili kuharakisha urasimkishaji wa sekta ya ardhi nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo mkoani morogoro.
Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri lukuvi
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri Lukuvi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...