
Vijana wa
Mujibu wa Sheria wanaotakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa ni wale wanafunzi wote waliomaliza kidato cha
sita mwezi Mei mwaka 2016, ambao hawakuchaguliwa kwenye mafunzo ya JKT Mujibu
wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya kwanza na hawakupata nafasi ya kujiunga
na vyuo vya elimu ya juu.
Iwapo kuna muhitimu
yeyote ambaye jina lake limetajwa kwenye orodha ya vijana wanaotakiwa kujiunga
na mafunzo ya JKT Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya pili na tayari
ameshajiunga na chuo cha elimu ya juu, anatakiwa kuandika barua ya kuomba kuhairisha
kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, akiambatisha vithibitisho vya yeye kuwa mwanachuo wa chuo
cha elimu ya juu.
Barua hiyo
itumwe kwa Mkuu Jeshi la Kujenga Taifa, Makao Makuu ya JKT, Sanduku la Posta
1694, Dar Es Salaam au iwasilishwe kwa mkono Makao Makuu ya JKT.
Aidha, JKT
inaukumbusha umma tena, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kijana yeyote
ambaye amechaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni
Magufuli awamu ya pili na amekaidi kuhudhuria mafunzo hayo bila ya sababu
zilizotajwa hapo juu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na
Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 13 Desemba 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...