Mkurugenzi
wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ,Dk.
Mwele Malecela akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya
taasisi hiyo jijini Dar es salaam leo akielezea mafanikio ya Taasisi
katika Mwaka 2016,katika nyanja mbalimbali ikiwmo Rasilimali na
uimarishaji wa utawala Bora,Usimamizi wa utafiti za Afya,Tafiti za Afya
ikinda sambamba na Matarajio yake kwa mwaka 2017
Baadhi ya Wadau na wataalamu mbalimbali pamoja na wanahabari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ,Dkt. Mwele Malecela alipokuwa akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yaliyohusu mafanikio ya Taasisi hiyo katika Mwaka wa 2016 pamoja na Matarajio yake kwa mwaka 2017.Picha na Michuzi Jr.
TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU
TAARIFA
KWA UMMA YA MAFANIKIO YA TAASISI KATIKA MWAKA 2016
Desemba 15,
2016
1.
RASILIMALI NA UIMARISHAJI WA UTAWALA BORA
Rasilimali fedha
Taasisi imeanzisha na kuanza kutumia mfumo wa fedha wa
kielektroniki. Mfumo huu unaendeshwa kwa pamoja na mfumo wa serikali wa
rasilimali watu. Ili kupanua matumizi ya mfumo huu mafunzo yametolewa kwa
wahisbu wote wa Makao Makuu na Vituo Vikuu vya Utafiti. Lengo ni kuunganisha
vituo vyote katika mfumo huo ili kurahisisha usimamizi wa mapato na matumizi ya
fedha za Taasisi.
Rasilimali watu.
Taasisi imeendelea kuwapa uwezo watumishi
wake katika ngazi mbalimbali za mafunzo. Watafiti 3 wameweza kuhitimu shahada
za uzamivu, 6 shahada za uzamili and 4 shahada ya kwanza katika kipindi hiki.
Taasisi imeshiriki katika utoaji mafunzo
kwa vitendo kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi. Watafiti
wa Taasisi wameshiriki kutoa mihadhara katika vyuo mbalimbali nchini – kama
vile Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbali mbali ikiwemo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Dodoma na taasisi nyingine
wamepata mafunzo katika maabara zetu. Pia taasisi imeendelea kuwasaidia
wafanyakazi wake kupata elimu ya juu katika ngazi za astashahada, shahada ya
kwanza, shahada ya uzamili na uzamivu. Watafiti watatu wametunukiwa shahada za
uzamivu katika mwaka 2016.
Mwongozo wa Matumizi ya Tehama
Taasisi
imeandaa Mwongozo wa Matumizi ya Tehama kwa ajili ya watumishi na wadau wake.
Mwongozo huo unapatikana katika tovuti ya taasisi (http://www.nimr.or.tz)
Uandaaji wa Takwimu-msingi
ya machapisho ya Taasisi
Katika kipindi cha 2016, Taasisi imeanza kuorodhesha machapisho yote ya
kitaaluma iliyochapisha katika kipindi cha uhai wake (1980-2016).
Takwimu-msingi hiyo itakuwa na machapisho ya majarida, vitabu na taarifa
nyingine za kisayansi. Takwimu-msingi itakapokamilika, watafiti watakuwa na
fursa ya kuongeza machapisho yao wenyewe kupitia tovuti ya taasisi. Hadi sana,
machapisho 1,249 yamehifadhiwa kwenye takwimu-msingi.
Matumizi ya Mifumo ya Taarifa za
Kijiografia
Taasisi imeendelea kujenga uwezo wa watumishi
wa afya kwa ngazi za mkoa na wilaya katika matumizi ya mifumo ya taarifa za
kijiografia. Jumal ya watumishi 230 kutoka
mikoa 16 na wilaya 107 wamepata mafunzo hayo. Kati ya hao, 214 wametoka katika
Wilaya na 16 kutoka mikoani
Huduma
za Maabara inayotembea.
Taasisi
imeendelea kutumia Maabara Inayotembea kutoa huduma za mafuzo katika Mkoa wa
Mbeya. Lengo ni kufikisha huduma za afya karibu na wananchi. Mafunzo yalitolewa
kwa njia mbalimbali, hususan kwa kutumia sinema. Magonjwa yaliyolengwa ni
UKIMWI na Kifua kikuu. Katika kipindi cha Oktoba 2015 hadi Oktoba 2016, Maabara
imeweza kuwafikia wateja 8,000; na asilimia 45% ya wagonjwa wa UKIMWI wameweza
kuunganishwa na huduma hiyo. Huduma nyingine zinazotolewa na maabara hiyo ni
kupima VVU, kupima chembechembe za damu za CD4, kupima Kifua Kikuu na saratani
ya shingo ya uzazi. Huduma ya uchunguzi wa usugu wa dawa za kurefusha maisha
(ARV) nayo imeongezwa katika huduma za maabara hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...