Timu ya michezo ya Bunge la Tanzania inashiriki katika toleo la saba la michezo ya Mabunge ya Afrika Mashariki iliyoanza mjini Mombasa, Kenya, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwenyekiti wa Timu ya Tanzania, Mhe. William Ngeleja, alisema kwenye kikao cha awali kabla ya ufunguzi rasmi wa michezo hiyo kilichofanyika Chuo cha Ufundi Mombasa jumapili, kuwa timu yake itakuwa na wanamichezo 60.
Mashindano hayo yanashirikisha mpira wa miguu, mpira wa pete, volleyball, gofu, kuvuta kamba na riadha kwa wanawake na wanaume. Baada ya ufunguzi rasmi uliofanywa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Fred Kadaga, Tanzania ilishiriki kwenye riadha wanawake na kuvuta kamba wanawake na wanaume. Mhe. Halima Mdee alishika nafasi ya pili mbio za mita 400 wakati Mhe. Esther Matiko alishika nafasi ya pili mita 400 na mita 100. Nafasi ya kwanza mbio zote mbili ilichukuliwa na Uganda.
Katika kuvuta kamba Tanzania wanaume walishindwa na Kenya wakati wanawake walishindwa na Uganda. Michezo hiyo inayoshirikisha nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki isipokuwa Sudan Kusini, yatamalizika Jumamosi Desemba 10.
Kiongozi wa Timu ya Tanzania, Mhe. William Ngeleja (kushoto) akishuhudia kukatwa keki wakati wa sherehe za ufunguzi wa michezo ya Mabunge kwenye Chuo cha Ufundi Mombasa.
Timu ya Bunge la Tanzania ikishiriki matembezi kuelekea uwanja wa Mamlaka ya Bandari ya Mombasa Mbaraki ambako michezo ya riadha na kuvuta kamba ilifanyika.
Timu ya Tanzania katika mitaa ya Mombasa wakati wa matembezi ya ufunguzi wa michezo hiyo.
Timu za Mabunge ya Afrika Mashariki zikishiriki matembezi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...