Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii
Mtandao wa Jinsia (TGNP) imeandaa warsha ya kuchangia sera
mpya ya ardhi kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kupitia fursa yake iliyopata kutoka
Wizara ya ardhi maendeleo na makazi ili kuweza kujua namna ambavyo jinsia
imeibuka katika kuchangia sera hii.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es Salaam,
Meneja Idara ya Ujenzi wa nguvu za pamoja Grace Kisetu, amesema kuwa katika
warsha hiyo wameweza kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika Halmashauri
wanazofanyia kazi zikiwemo Kishapu,Morogoro,Mbeya,Mara na Shinyanga pamoja na asasi zisizokuwa za kiserikali na
wanajamii kutoka sehemu ambazo tunafanyia kazi na baadhi ya washiriki kutoka
wizra ta ardhi.
“Tumeamua kuwashirikisha wadau hao ili waweze kutusikiliza
na kujua chambuzi ambazo tumeweza kuzifanya ili waweze kujua ni lipi tunaloliona
kwamba kwenye rasimu walioitoa pengine linahitaji kuboreshwa zaidi hususani
tukiangalia je jinsia ni ninsi gani imechukuliwa na kuweza kujitokeza kwenye
hiyo sera ya ardhi ya mwaka 2016”
Kwa upande wake Muwezeshaji wa warsha hiyo Magdalena
Luwevangila ameongeza kuwa katika Warsha hii tunaangalia jinsi gani sera
inaweza ikakidhi mahitaji ya watu wote hususan katika masuala ya
kijinsia,wanawake watoto,wanaume na watu waliopo pembezoni ili iweze kufanya
kazi na kumaliza migogoro ya ardhi mara tu inapojitokeza.
” migogoro ya ardhi inayojitokeza hasa kwa upande wa rushwa
ambapo serikali za vijiji zimeshindwa kusimamia tatizo hili na badala yake
ubadhilifu umekuwa mwingi, hivyo sera hii ijikite katika kutatua na kuondoa
migogoro hiyo”.
Nae mmoja wa wadau ambaye ni Mkulima kutoka Mkoa wa Mara Kata ya Nyakonga, Nyangi
Marwa ameiomba serikali kuwaangali wanawake na wajane waliopo pembezoni kwani wengi wao hawajui haki
zao juu ya umiliki wa ardhi ili kuepuka kunyanyasaji hasa katika kipindi cha
mirasi.
TGNP ni shirika ambalo lipo mstari wa mbele katika
masuala ya kijinsia na imepata nafasi ya kuweza kuchangia katika suala zima la
sera mpya ya ardhi , ambapo kutokana na warsha hiyo TGNP inatarajia kutengeneza
kikosi kazi cha Taifa Kitakachoundwa na wadau mbalimbali ambacho kitaongeza
nguvu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sera hizi ili kuongeza nguvu kwenye ushawishi na utetezi
wa usawa wa kijinsia hususan utekelezaji wa sera zetu .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...