Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Cliford Tandari
(kulia) akisaliama na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania
Cereramics, Jack Feng wakati alipotembea eneo litakalojengwa kiwanda
kikubwa cha kutengeneza "Tiles" Desemba 14, 2016 lililopo katika Kijiji
cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. TIC ilitembelea eneo hilo, ikiwa ni
utaratibu wake iliyojiwekea wa kuwatembelea wawekezaji wote nchini na
kuona maedeleo ya uwekezaji walioomba kama unafanyika kama walivyoomba.
Ujenzi wa kiwanda hiki unatarajiwa kuanza mapema mwezi Januari 2017 na
zaidi ya Watanzania 6000 wataweza kupata ajira kupitia kiwanda hiki.
Kabla ya kutembelea mradi huo, Tandari aliembatana na baadhi ya
watendaji wa TIC alitembelea eneo lingine linalotarajiwa kujengwa
kiwanda cha kutengeneza sabuni, kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani.


Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng akieleza
jambo mbele ya wanahabari pamoja na Ujumbe wa TIC wakati wa ziara ya
kutembelea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza "Tiles" Desemba 14,
2016 lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...